MACHAFUKO NCHINI BURUNDI TANZANIA YAANZA KUPATA ATHARI ZAKE,SOMA HPO KUJUA

ATHARI za machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini Burundi yamenza kuigusa Tanzania,baada ya wakimbiza wanaokimbia machafuko hayo kuja Mkoani Kigoma wamesebabisha kuibuka ugonjwa mkubwa wa kipindupindu na kusababisha vifo vya watu 10 mpaka sasa.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam
na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Steven Kabwe Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari
ambapo amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu mkoani
Kigoma pamoja na mashirika mbali mbali
ya Kimataifa ya kuwahudumia Wakimbizi wamethibitisha kutokea na Vifo hivyo
ambapo vyote vimetokana na Ugonjwa wa Kipindupindu.
“Kwa sasa
tumethibitisha pasipo shaka watu 10 wamekufa kutokana na Ugonjwa wa
kipindupindu na baada ya kufanya uchunguzi ambao tulishirikiana na mashirika ya
Kimataifa tumebaini sehemu kubwa ya Ugonjwa huu umetokana na ujio wa wakimbizi
kutoka nchini Burundi”amesema
Kwa Mujibu
wa Naibu Waziri Kabwe amesema Mpaka jana Teyari walikuwa wameshawapokea
wakimbizi Laki mbili kutokea Burundi ambapo anasema kutokana na Ufinyu wa
maeneo ikiwemo matumizi ya Maji pamoja na uchache wa huduma za choo ndio
imekuwa miongoni mwa sababu ya kuibuka Ugonjwa huo.
Pamoja na
hayo amebainisha kuwa kwa sasa hatua
ambazo Serikali imechukua za haraka ni kuwapeleka madaktari pamoja na huduma
mbali mbali za kibanadamu ili kuweza kuokoa Tatizo hilo kubwa.
Aidha,Muheshimiwa Kabwe akawataka
Waganga wakuu wa mikoa nchi nzima pamoja na Wananchi kuchukua tahadhari ikiwemo
kuweka maeneo safi.
No comments
Post a Comment