HABARI KUBWA LEO,MGOMO MKUBWA WANUKIA,NI WANAFUNZI VYUO VIKUU,WAAPA KUINGIA BARABARANI MDA WOWOTE,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Picha ni kutoka maktaba yetu. Wanafunzi wa UDSM wakiandamana |
WAKATI
Serikali ikitarajia kusoma Bajeti ya mwaka 2015-2016 Bunge Mkoani Dodoma,Wanafunzi wa Vyuo vikuu mbali mbali nchini wametangaza
kuanza mgomo mda wowote kuanzia sasa kuishinikiza Serikali iwalipe pesa na
kujikumu za kila siku ambazo zilitengwa kwenye Bajeti wa
2014-2015.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mtandao huu Wanafunzi
mbali mbali kutoka Vyuo Vikuu tofauti nchini ambapo wamesema wameshindwa kuelewa na Ukimya wa Bodi ya Mkopo nchini kwa kushindwa kuwapatia Fedha za kujikimu kwa zaidi ya Miezi miwili sasa
na kusema kuwa hawaoni Haja ya kuendelea kuingia madarasani kusoma.
Akizungumza Kwa Jazba Mwanafunzi wa
Shahada ya sheria kutoka chuo kikuu cha Mlimani amesema hawana sababu ya
kuendelea kukaa darasani kwani mpaka sasa pesa ya kula waliokuwa nayo imekwisha
vilevile wakiandamwa na madeni makubwa
kutoka kwa wanafunzi wenzao.
“Tumeichoka hii Serikali kwanini
haitujali sisi wasomi bwana maana tumekaa bila hata kula kwa siku nzima mpaka
sasa hatujapewa pesa zetu kwa mda wa miezi miwili, mpaka sasa unategemea nini?,na
hatupewi majibu ya kujitosha,bora tugome tu maana hatuna jinsi’alisema
mwanafunzi huyo.
Nao, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Tumaini kilichopo Mkoani Arusha
wametishia kugoma kutokana na kutopewa
Pesa hizo.
“Tumevumilia
tumechoka bora tugome watu hatuna pesa za kijikimu na mitihani ya kumaliza
mwaka imekaribia hivi wanazani tunaishiji? Kama hawa wakina dada zetu huku wanafanya
Ngono wapate pesa wewe unategemea nini bora tugome hii serikali tumeichoka
bwana”Wamesema mwanafunzi wa hao.
Bodi ya Mikopo wanena.
Akizungumza
kwa sharti la kutotaja jina lake mtandaoni Ofisa mmoja wa Bodi ya Mkopo amesema
kuwa Kama watu wanaotakiwa kupewa lawama
kwenye sakata hili sio wao Bodi ya
Mikopo bali ni Serikali yenyewe.
“Serikali
sahivi haina Pesa kabisa,watu wawe wanona wakuwapa Lawama, leo Serikali Pesa zake zimeelekezwa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) kwenye Masuala ya BVR sasa wao wanataka kumlahumu nani, hapa
bwana wafuate Serikali yao”amesema
No comments
Post a Comment