MWANDISHI KUBENEA AWACHUKIZA VIONGOZI ACT-WAZALENDO,MWIGAMBA ASEMA HAYA
Pichani ni KATIBU MKUU WA CHAMA CHA ACT-WAZALENDOSAMSON MWIGAMBA PICHA NA MAKTABA |
KILE
kinachoonekana ni kama Viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wamesindwa kuvumilia juu ya Makala Mfululizo zinazoandikwa na Mwandishi Saed kubenea kwenye Gazeti la
Mawio kuhusu mwenendo chama hicho.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Baada ya Hivi sasa viongozi wa
Chama hicho kichanga cha siasa nchini kuibuka na kusema uvumilivu utafikia
mwisho na kutishia kumfikisha Mahakamani Mmiliki wa Gazeti hilo pamoja na
Mhariri wake.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa
Chama hicho Samson Mwigamba wakati akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu
kwenye Semina iliyoaandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC)
iliyowakutanisha wanasiasa mbali mbali wa vyama vyote vya Siasa nchini kujadili
mambo mbali mbali kuelekea uchaguzi Mkuu hapo baadae mwaka huu ambapo-
Mwigamba akizungumza kwa uchungu amesema
kwa sasa viongozi wa chama hicho wanasikitishwa na Uandishi ambao wanadai ni wa
kutumiwa na watu wenye mapenzi mabaya na ACT-Wazalendo kwa kuandika Makala
zilizojaa uwongo.
“Hivi ule ni uwandishi wa aina gani,maana
inasikitisha kuona miezi zaidi ya mitatu mwandishi na Mhariri wanaandika habari moja
tu yaani kila siku na ACT-Wazalendo tena kwa mabaya yaani hawajawai kuandika
makala zinazohusu mazuri,wao ni mabaya tu na hayo mabaya ni ya uongo hayana
ukweli ,lakini uvumilivu unamwisho nakwaambia tutachoka na sisi tutakwenda hata
mbele ya Sheria”amesema Mwigamba.
Mwigamba
ambaye kabla ya kuwa ACT-Wazalendo alikuwa kiongozi wa Chadema Mkoani Arusha na
alifukuzwa Viongozi wa chama hicho kwa madai ya kuandaa mipango ya kuhujumu
chama hicho Kikuu cha Upinzania nchini.
Kuibuka huko kwa Mwigamba kunakuja ikiwa
umepita mwezi mmoja baada ya Kiongozi
Mkuu wa ACT-Wazalendo nchini Zitto Kabwe kumtuhumu Mmiliki wa Gazeti la Mawio
ambaye Kabwe anasema ndio mmilikiwa Mtandao wa Mwanahalisi.oline kuandika
Habari ambazo Zitto anazidi dai kuwa zilikuwa zina lengo la kumgombanisha na
Mwenyekiti wa IPP Bwana Mengi.
No comments
Post a Comment