HABARI KUBWA LEO.MAJIMBO KUGAWA UPYA,SASA WABUNGE KUONGEZEKA MARADUFU KURIKO WA SASA,PROF LIPUMBA ALIA NA NEC SOMA KUJUA

TUME ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), imepanga kuyagawa upya majimbo ya uchaguzi nchini. Mwenyekiti
wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema, tume yake tayari imekamilisha
ugawaji majimbo hayo na muda wowote itaanza mchakato wa kuyagawa. Anaandika
Sarafina Lidwino … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam, Jaji Lubuva amesema, tume yake imeamua kugawa majimbo
hayo kwa kuzingatia vigezo mbalimbali, ikiwamo idadi ya watu, upatikana wa
mawasiliano, hali ya kijiografia na alichoita, “kanuni za uchaguzi wa Rais na
wabunge ya mwaka 2010.”
Aidha, Jaji Lubuva amesema, Tume itayagawa majimbo hayo kwa kuzingatia
uwepo wa miundo mbinu bora, hali ya kiuchumi kwa kuweka uwiano kati ya eneo
moja na jingine, simu na vyombo vya habari kwa ajili ya kupata mwakilishi atakae
harakisha maendeleo katika eneo husika.
NEC inatangaza majimbo mapya ya
uchaguzi, huku uandikishaji wa wananchi katika daftari la kudumu la wapigakura,
ukiwa umedolola.
Amedai kuwa kuna baadhi ya majimbo ni
makubwa kulinganisha na majimbo mengine, jambo ambalo linatokana na ongezeko la
watu nchini.
“…zoezi hili linatakiwa kufanyika mara
kwa mara au angalau mara moja baada ya miaka 10. Ugawaji wa majimbo ulifanyika
katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, na kwa kuwa sasa tunaelekea katika uchaguzi
mwingine, lazma tufanye hivyo,” ameeleza Jaji Lubuva.
Amesema utaratibu utakaotumika
katika ugawaji wa majimbo hayo na kubadilisha mipaka, ni kuwasilisha maombi ya
kufanya hivyo, yawasilishwe kwa Mkurugenzi wa Halmashauri, kwenda kwa katibu
tawala, katibu tawala za mikoa, kisha kwenda NEC.
Hata hivyo, mara baada ya kuwasilishwa
maelezo hayo, baadhi ya wajumbe kutoka vyama vya upinzani wadai kuwa ugawaji
huo wa majimbo unafanyika kwa shinikizo la Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Tume imezidiwa na majukumu; wanataka
kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja, huku muda ukiwa haupo,” alisema Prof.
Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF).
Alihoji, “walikuwa wapi siku zote,
wakati muda uliobaki hautoshi?”
Chanzo changu kilipomuuliza,
Dk. Emmanuel Makaidi, mwenyekiti wa chama cha National League Democrat (NLD)
amesema, “NEC inafanya kazi za CCM.”
Akiongea kwa
uchungu, Dk. Makaidi amesema, “Hii ni tume inapangiwa kazi na serikali, siyo
kujipangia. Ni tume mbovu kuliko ile ya Jaji Luis Makame.”
Chanzo ni Gazeti la Mwanahalisi.oline
No comments
Post a Comment