Zinazobamba

HABARI KUBWA LEO.WAZIRI MAGUFULI AMTIA KIWEWE LOWASSA,KAMBI YAKE YAJITOSA KUPAMBANA,SOMA HAPO KUJUA

Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli Bw.Edward Lowassa akikabidhiwa mkuki kama ishara ya kukabidhiwa majukumu ya kuwa mlezi wa Machifu Tanzania
Pichani ni Edward Lowassa

SIKU moja kupita baada Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli kutangaza Rasmi kujitosa kwenye nafasi ya Urais ndani ya chama cha Mapinduzi CCM,kunatajwa kuiweka kiwewe kambi ya Edward  Lowassa ambaye anautaka Urais kwa udi na Uvumba ndani ya Chama hicho,Mtandao huu umebaini.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
       Dk. Magufuli, mmoja wa mawaziri ambao kwa muda mrefu wamehusishwa kwenye kinyang’anyiro cha nafasi hiyo, alisema anaingia kwenye mchuano huo akiwa na sifa zote stahiki za kupiga na kupigiwa kura.
       Alitangaza azma yake nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, muda mfupi baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu bungeni, jana asubuhi.
     
         Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu umezipata kutoka ndani ya Kambi ya Lowassa ambaye ni Waziri mkuu aliyejiuzulu kutokana na Kashfa ya Ufisadi kwenye Kampuni Tata  ya Richmound zinasema kwa sasa kambi hiyo imejipanga kuhakikisha kumwandalia mipango ya Kumchafua kwa Wajumbe wa Halmashauri kuu NEC ili jina lake lisipite.
        Lowassa ambaye kesho anatarajia kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais ndani ya Chama hicho , mkoani Arusha kwenye Uwanja Sheikh Aman Abed Karume na kurushwa moja kwa moja (Live) na Luninga zaidi ya tatu sanjari na Redio zaidi ya tano,
       Mbali na kutangaza huko nia yake ya Urais ndani ya chama chake pia Lowassa anatajwa pia kuliweka bayana suala na Mkataba wa Kinyonyaji wa Richmound.
       Akizungumza kwa sharti la kutaja jina lake Mjumbe wa Kamati wa Kambi ya Lowassa  amesema kutangaza nia kwa Waziri Magufuli kumeleta msuguano ndani ya kambi hiyo.
    “Sikiliza  ndugu sahivi kambi ya mzee (Lowassa) imepata mtikisiko  mkubwa sana baada ya kusikia nae magufuli anautaka Urais kiukweli  mambo yatakuwa magumu”amesema Mjumbe huyo.
         Sababu ambayo inatajwa na wajumbe hao kwa Magufuli inatokana na hazi aliyokuwa nayo kwenye jamii ikiwemo kasi yake ya aliyoonyesha ndani ya wizara alizoziongoza ikiwemo Wizara anayongoza sahivi  ya Wizara ya Ujenzi.
“Huyu bwana kiutendaji yupo vizuri sana,tena anaonekana ni mtu wa maamuzi mazuri,harafu anauchungu na watanzania mbali na hivyo pia hata watanzania wanamkubali kwani ana viashilia vya udikteta na Taifa linaitaji mtu kama huyo na ndio maana kambi ya Lowassa inakuwa na wasi wasi”ameeleza mchambuzi wa siasa kutoka Dar es salaam.
      WAJUMBE WA NEC WANENA.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM (NEC)waliozungumza na Mtandao huu wameoneshwa kuchukizwa na kitendo cha Lowassa kuunda “utatu mtakatifu” na watu ambao wanatajwa kuhusika kwenye kashfa mbali mbali za Ufisadi.
“Mimi mwenyewe nilikuwa mtu wa lowassa ila kwa sasa nimekata tama na kusema huyu mtu afai ndani ya nchi hii,leo nashangaa sana anashirikiana na watu mafisadi kama wakina Rostam,Chenge,Karamagi,watu ambao wameliangamiza Taifa hili kwa ufisadi wao,harafu leo ndio watu wake wewe unategemea nini”amesema Mjumbe wa NEC kutoka mkoani Mbeya.
     Dk. Magufuli, amekuwa mbunge tangu mwaka 1995 aliyasema hayo Baada ya kuulizwa kama ana mpango huo, mara moja alisema: “Swali hili nimeulizwa mara nyingi. Mara zote nimekataa kulijibu kwa sababu chama chetu (CCM) kuna utaratibu wake wa namna ya kuomba nafasi ya uongozi. Muda ulikuwa haujawadia.
       “Lakini utakumbuka wiki hii hapa hapa Dodoma, vikao vya juu vya chama chetu vimetoa ratiba kwa wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali kujitokeza.
       “Kwa maana hiyo sasa niko huru kujibu swali lako kwa kusema rasmi ‘nitagombea urais’. Nafanya hivyo kwa sababu naamini ninazo sifa za kuchagua na kuchaguliwa kama mwanachama wa CCM kwa nafasi yoyote inayojitokeza kulingana na Katiba ya chama chetu na pia Katiba ya nchi,” alisema Dk. Magufuli.
       Alisema siku ya kuchukua fomu ataitangaza baadaye pindi akishakamilisha taratibu za namna ya kuanika hadharani mambo anayokusudia kuyatekeleza endapo wana CCM watampa ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho.


      

Hakuna maoni