HABARI NJEMA TOKA PPF,YANYAKUA TUZO BORA DUNIANI,SOMA HAPO KUJUA
pichani ni Mkurugenzi wa PPF Wiliam Erio picha na Maktaba
MFUKO wa
Hifadhi ya Jamii PPF imezidi kukubalika katika Nyanja za kimataifa baada ya
kutunukiwa tuzo ya Ubora wa Kutoa Huduma inayojulikana Internatonal Standard Organization (ISO)
kutokana na huduma zinazotolewa.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Akithibitisha
kupokea kwa Tuzo hiyo leo Jijini Dar es Salaam
Mkutano na Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Mfuko huo Wiliam Erio
wakati wa ambapo amesema sababu iliyochangia kupata Tuzo hiyo inatokana na
Huduma bora ambazo zinatolewa na PPF kwa jamii hususani wafanyakazi na
watumishi mbali mbali ikiwemo hadi kwenye Sekta Binafsi.
Pamoja na
hayo amebainisha kuwa Nishani hiyo ya Kimataifa waliopewa haitowafanya
kubweteka katika kutoa huduma badala yake amesema wataongeza Juhudi katika
kutoa huduma kwa Jamii jambo ambalo anadai kuwa litaipanua serikali katika
miradi mbali mbali.
Sanjari na
hayo Bwana Erio amesema kuwa kwa sasa wataje wa Mfumo wa PPF wategeme kupata
Huduma bora na za kisasa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni