YAMETIMIA CHADEMA--UCHAGUZI WAKE WA NDANI NI PASUA KICHWA,HAWA NDIO WALIOJITOSA SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
![]() |
| PICHANI NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA FREEMAN MBOWE PICHA NA MAKTABA |
Na Janet
Josiah
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
kimetoa orodha ya wanachama wake waliojitosa kugombea nafasi mbalimbali za
taifa katika mabaraza huku mnyukano mkali ukiwa nafasi za mwenyekiti, makamu
mwenyekiti, katibu mkuu, naibu katibu mkuu na uenezi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam jana, Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uratibu wa Kanda,
Benson Kigaila, alisema katika baraza la vijana, wanawake na wazee, nafasi hizo
zimepata wagombea zaidi ya watano.
Kigaila,
alisema kwa upande wa Baraza la Wanawake (Bawacha), wanachama sita wamejitokeza
kuwania uenyekiti akiwamo Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Lilian Wassira, Sophia
Mwakagenda, Rebeca Magwisha, Diwani wa Kunduchi, Janet Rite na Mbunge wa viti
maalum
, Chiku Abwao.
Nafasi ya Makamu
Mwenyekiti Bawacha Bara (1), na Visiwani (1), waliogombea wako sita ambao ni
Sina Manzi, Victoria Tindabatangile na Hawa Mwaifunga wakati kwa upande wa
Zanzibar ni Hamida Abdalah, Nasra Jusha Barwan na Mbunge wa Viti maalum,
Mariamu Salum Msabaha anayetetea nafasi hiyo.
Kwa upande
wa Katibu Mkuu Bawacha waliogombea wako sita, Catherine Vernand, Grace Tendega,
Anna Mughwira, Nagy Kaboyoka, Mbunge Viti maalum Paulina Gekul na Mbunge Viti
maalum, Naomi Kaihula anayetetea nafasi hiyo.
Waliogombea
nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara (1), na Visiwani (1) wako watano ambao ni
Clara Mayuki na Yudith Mchaki wa Visiwani wakati Bara ni Ester Daffi, Florence
Makazigwa na Kunti Majala.
Katika Baraza
la Vijana la CHADEMA (Bavicha), walijitokeza nafasi ya mwenyekiti wako 13,
ambao ni Daniel Naftal, Upendo Peneza, Pachal Patrobas, Ephata Nanyaro, Freddy
Hatari, Filipo Mwakitinge, Mruta Masolwa, Godfrey Bagamba, Meshack Michael,
Lazoro Kapinga, Mussa Mabawa, Alex Thomas na Joseph Mashinga.
Waliogombea
nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bavicha Taifa Bara nafasi (1), na Visiwani (1),
wako 15 akiwamo Johnson Luzibukya, Aggrey Dud, Ibrahim Bashe, Khalid Ausi,
Julieth Lushuli, Nusrtat Hanje, Jane Nyamsenda, Jesca Kishoa, Rose Mayemba,
Zainab Ashraff, Patrick Kpura, Sharif Suleman Hamis, Francis Werema, Zendi
Marano Abdulahi na Shaban Omary Shaban.
Nafasi ya
Katibu Mkuu wa Bavicha Taifa imegombewa na wanachama 10 ambao ni Fahamu Juma,
Alphonce Mwamwile, Goodluck Moreli, Paulo Makuli, General Kaduma, Benson
Mramba, Methew Kishili, Meo Benard, Salim Mpanda na Julius Mwita.
Kwa upande wa
nafasi ya Uhamasishaji/Uenezi wa Bavicha Taifa waliojitokeza ni Julius Kapunda,
Daniel Sanga, Musaa Ndile, Edward Simbeye, Moses Mwaifunga, John Lutulagala,
Francis Marwa, Pina Baharia, Baraka Mfilinge, Amina Saguti, Justine Simon na
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassary.
Baraza la Wazee
waliojitokeza kugombea nafasi ya mwenyekiti ni Kayaga Ismale Kayaga, Hashimu
Juma Ismal, Jacok Qorro, Njomba Koi na Arcado Ntagazwa.
Waliogombea
nafasi ya Makamu Mwenyekiti Wazee ni pamoja na Kwaio Hamis, Omary Masoud Omary,
Suzan Lyimo (mbunge viti maalum), Clavery Ntidicha, Othma Haule na Omary Juma
Mkama.
Pamoja na
majina hayo, Benson alitaja majina na nafasi za wanachama wao katika mabaraza
wanayogombea nafasi ya katibu mhamasishaji, mweka hazina, wajumbe wa tano
kuingia katika baraza kuu na wajumbe 20 kuingia mkutano mkuu wa taifa wa
CHADEMA.
Hata hivyo, alisistiza kwamba, uchaguzi wa mabaraza utaanza
Septemba 6 kwa Baraza la Wazee, Septemba 10 Bavicha na Bawacha Septemba 11
mwaka huu.
“Septemba 12
kamati kuu ya zamani itakaa kuandaa kikao cha Baraza Kuu jipya ambalo
litakutana Septemba 13 kupitisha marekebisho ya vifungu vya katiba na kuandaa
mkutano mkuu ambao utafanyika Septemba 14 mwaka huu.
“Baraza kuu
litakaa tena Septemba 15 kwa ajili ya kutunga kanuni za kutekeleza vifungu
vilivyopitishwa katika mkutano mkuu na kumchagua katibu mkuu, naibu katibu mkuu
bara na visiwani pamoja na kuwachagua wajumbe wa kamati kuu,” alisema Benson

No comments
Post a Comment