MASIKINI LOWASSA,SASA CCM YAVUNJA RASMI MTANDAO WAKE WA URAIS,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
![]() |
| Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana |
Na ELIYA
MBONEA, ARUSHA NI MWANDISHI WA GAZETI LA MTANZANIA
KATIKA kile kinachoonekana ni kuvuruga kambi
za wagombea urais mwaka 2015, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepangua makatibu wa
mikoa 17 kwa kuwahamisha vituo vyao vya kazi.
Makatibu hao ni pamoja na Mary
Chatanda aliyekuwa Mkoa wa Arusha, ambaye kwa sasa amehamishiwa Singida.
Chatanda kwa muda mrefu amekuwa na
msuguano ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Arusha, huku kiini chake
kikidaiwa ni misimamo tofauti ya vijana hao kumuunga mkono Mbunge wa Monduli,
Edward Lowassa ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa watakaoomba kugombea urais
kupitia chama hicho mwakani.
Wachambuzi wa masuala ya siasa
ndani na nje ya chama hicho tawala, wanaona hatua ya kupangua idadi kubwa ya
watendaji wa mikoa huku kukiwa kumebakia miezi michache kinyang’anyiro cha
kugombea kuwania urais kuanza mwakani, inalenga kuvunja mitandao ya urais au
njia ya kujipanga na uchaguzi mkuu.
“Kuna mambo mawili makubwa, CCM ama
inavunja mitandao ya urais iliyojengwa na watendaji hawa, au inajipanga kwa
ajili ya uchaguzi mkuu wa mwakani,” alisema kada mmoja ambaye hakutaka kutajwa
jina lake.
Alisema panguapangua hii ya Katibu
Mkuu Abdulrahman Kinana, ambaye anachukuliwa kama mtu muhimu ndani ya chama
hicho katika kushinda chaguzi mbalimbali, inaweza ikawa imebeba siri kubwa.
Kwa mujibu wa barua hiyo yenye
kumbukumbu namba CMM/OKM/M.11/Vol.7/1, yenye kichwa cha habari “Uhamisho wa
Makatibu wa Mikoa” iliyosainiwa na Kinana Septemba Mosi, Alphonce Kayanda,
amehamishwa kutoka Mkoa wa Katavi kwenda Arusha.
Barua hiyo, inaonyesha kuwa Joyce
Kasunga amehamishwa kutoka Mwanza kwenda Pwani,na Janeth Kayanda anatoka
Bukoba Mjini kwenda Tabora.
Kinana aliwataja wengine ni Gustav
Muba anayehamia Geita kutoka Tanga, Sauda Mpambalyoto anayekwenda Kusini Unguja
akitokea Pwani na Evelyine Mushi anayetoka Kagera kwenda Katavi.
Makatibu wengine wanaohamishwa
vituo vyao vya kazi ni Naomi Kapambala anayetoka Singida kwenda Kigoma, Idd Ame
kutoka Tabora kwenda Kagera na Shija Othman Shija ambaye anatoka Kusini Pemba
anakwenda Tanga.
Uhamisho umewagusa pia Mwangi R.
Kundya kutoka Mjini Magharibi kwenda Mbeya, Mohamed Nyawenga anatoka Kigoma
kwenda Mjini Mangaribi, Adam Ngalawa anatoka Shinyanga kwenda Mara na Maganga
Sengelema anatoka Mbeya kwenda Shinyanga.
Wengine ni Zainab Shomari anayetoka
Kusini Unguja ambaye kwa mujibu wa barua hiyo amepewa likizo miezi miwili, Mary
Maziku anatoka Geita anakwenda Makao Makuu Dodoma na Bernad Nduta anatoka Makao
Makuu anakwenda Mwanza.
Kutokana na uhamisho huo na hasa kwa
Katibu wa CCM Arusha, Chatanda, MTANZANIA lilitafuta maoni ya wadau wa siasa
ili kujua wanazungumziaje kuhusu uhamisho wake.
Kwa upande wake, Kada wa CCM mkoani
Arusha ambaye hakuwa tayari jina lake kuandikwa gazetini, aliliambia MTANZANIA kwamba
uhamisho huo ni wa kawaida wa kikazi.
“Siasa ni mchezo wa makundi, hivyo
siamini kama kuondoka kwake vurugu zilizokuwa ndani ya CCM hapa Arusha
zitaisha. Tofauti lazima ziendelee.
“Lakini kwa upande mwingine naamini
itatuletea amani kwa CCM hapa Arusha japo hatujui anayekuja ana tabia zipi na,
kwani inaweza ikawa afadhali anayeondoka kuliko ajaye,” alisema kada huyo.
Tangu Chatanda ahamishiwe Arusha
hali ya kisiasa mkoani humo imekuwa ni ya vuta nikuvute baina ya CCM na vyama
vya upinzani na wakati mwingine ndani ya chama hicho tawala.
Juhudi za MTANZANIA kupata
ufafanuzi wa viongozi wa juu wa CCM kuhusu uhamisho huo ziligonga mwamba hadi
tunakwenda mitamboni baada ya simu ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania
Bara, Philip Mangula simu yake kuita na kukatwa huku ya Katibu wa Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye ikiita bila kupokelewa

No comments
Post a Comment