TLS, IBA WAWAKUTANISHA WANASHERIA PANDE ZOTE DUNIA KUJADILI RASILIMALI YA MADINI, MKUTANO HUO UTATOA SULUHUSU YA MIKATA MIBOVU
| Nafanua zaidi, wakili huyo akifafanua zaidi |
DARESALAAM
Tanzania kupitia chama
cha wanasheria cha Tanganyika law society (TLS) inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano
mkubwa wa aina yake wenye lengo la kujadili fulsa na changamoto za kisheria
zinazoikabili sekta ya madini katika bara la Afrika hivi karibuni
Akizungumza na
waandishi wa habari mapema hii leo, muandaji wa mkutano huo ambaye pia ni
mjumbe wa Tanganyika Law Society Wakili Daniel WEL WEL amesema, mkutano huo
umekuja kufuatia kuonekana kwa unyonyaji wa mikataba mbalimbali ya kisheria inayofanywa
na wawekezaji katika sekta ya madini
Wakili Wel Wel
ameendelea kusema kuwa kwa muda mrefu Tanzania kumekuwa na vilio kuhusiana na
mikataba kwa sekta ya madini ,hivyo ujio wa mkutano huo utasaidia kwa kiasi
kikubwa kujua wenzetu katika mabara mengine duniani wanafanya nini mpaka
rasilimali zao zinaweza kuwanufaisha,
Naye katibu mkuu wa
chama hicho cha (TLS) Wakili Alphonce Gura ametaja Baadhi ya Changamoto ambazo
zitaangaliwa kwa kina katika mkutano huo kuwa ni pamoja na zile za
kisheria,kiuchumi na za kimazingira ambazo mara nyingi zimekuwa zikiwaathiri
wakazi walio karibu na mazingara ya uchimbaji wa madini
Akielezea sababu za
chama cha wanasheria duniani (IBA) kukubali kupeleka mkutano huo Tanzania, wakili
Gura amesema fulsa hiyo imekuja kufuatia mwenendo mzuri wa ukuaji wa uchumi wa
taifa na kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa sekta ya madini hapa nchini
Katika mkutano huo
unaotarajiwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali toka kila kona ya dunia utahusisha
jumla ya washiriki 150 ambao watajadili ni namna gani wanaweza kulisaidia bara
la Afrika kuondokana na tatizo la kisheria katika sekta hiyo ya madini, na
kwamba mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Naibu waziri wa nishati
na madini
MAGALLI………………PRESS………………..03/09/2014
No comments
Post a Comment