Zinazobamba

KUHUSU TAARIFA ZA MWANDISHI KUBENEA KUPIGWA RISASI,HUU NDIO UKWELI ULIVYO,SOMA HAPA KUJUA


Pichani niSaed Kubenea,
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited - wachapishaji wa gazeti la MwanaHALISI, lilosimamishwa na serikali kwa muda usiojulikana, MSETO, MwanaHALISI Online.com na mtandao wa MwanaHALISI Forum pamoja na
sasa niMwandishi wa Gazeti la Mawio Picha na Maktaba

Na Karoli Vinsent
KUFUATIA taarifa mbalimbali zilizokuwa zimezushwa na kusambazwa kwenye simu pamoja na Mitandao ya kijamii kwamba Mwandishi Mwandamizi na Mzalendo wa Nchi yake, Saed Kubenea amepigwa Risasi na hali yake kuwa mbaya,sasa hivi ndivyo  mwenyewe alivyojibu
       "Taarifa zimetupwa kwenye mitandao ya simu, zikisema kuwa mimi Saed Kubenea, nimejeruhiwa kwa risasi na kwamba hali yangu ni mbaya sana. Imeelezwa kuwa tukio hilo lilitokea leo majira ya saa tano asubuhi katikati ya jiji la Dar es Salaam.


Binafsi nimejulishwa tukio hilo na Mwandishi wa habari wa Star TV na baadaye nikaelezwa kuwapo uvumivu huo na Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Neville Meena.

Napenda kuujulisha umma kuwa habari hizo siyo kweli. Mimi niko salama na naendelea na majukumu yangu kama kawaida”alisema Kubenea
Ikumbukwe Kubenea ni Mwandishi wa Gazeti la Mawio na mmiliki  , MwanaHALISI Online.com na mtandao wa MwanaHALISI Forum pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited - wachapishaji wa gazeti la MwanaHALISI, lilosimamishwa na serikali kwa muda usiojulikana, MSETO,ambapo kubenea ambaye amefungua kesi Mahakama kuu kushinikiza Bunge Maalum la Katiba livunjwe kutokana na bunge hilo kupoteza pesa za Watanzania

No comments