Zinazobamba

MAKAME MBALAWA AZINDUA HUDUMA ZA MATIBABU KWA NJIA YA MTANDAO HUKO bAGAMOYO


Waziri wa mawasiliano sayansi na Teknolojia akifafanua jambo mbele ya wadau wa huduma mtandao ambao wamehudhulia katika mkutano wa siku mbili huko mjini Bagamoyo kujifunza kuuhusu mradi mpya wa matibabu kwa njia ya mtandao. Mradi huo mpya unatarajiwa kuwasaidia kwa kiasi kikubwa watanzania kutokana na ukweli kuwa ni huduma ambayo hutolewa kwa haraka
Wadau waliiohudhulia mkutano huo wakiwa makini kusikiliza kile kinachoelezwa na mh. Waziri Makame.Huduma hiyo ya matibabu kwa mtandao itamsaidia mgonjwa kupata matibabu kwa haraka tena katika hosipitali ambayo iko karibu yake,ni huduma ambayo mteja ataifuata katika hospitali kama kawaida ila katika hospitali hizo daktari ataweza kuwasiliana na madaktari wengine waliiobobea katika magonjwa mbalimbali kwa njia ya mtandao ili kumsaidia mgonjwa

kulia ni Muheshimiwa waziri, Makame Mbalawa na kushoto ni Mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa umma, Eng. Peter Ulanga wakiwa katika mkutano huo

CEO wa mfuko wa mawasiliano kwa umma akifafanua jambo kwa wadau wa mkutano huo kuhusu, mfuko wa mawasiliano kwa umma umelenga kutoa fursa kwa watanzania kupata mawasiliano kwa haraka na ya uhakika, kupitia mfuko huo matibabu kwa njia ya mtandao inawezekana. Mfuko huo ulianzishwa rasmi mwaka 2006 na rais wa jamuhuri ya muungano wa TANZANIA Mh. Jakaya Mrisho Kkikwete na kuanza kufanya kazi rasmi mwaka 2012.



Picha ya pamoja ya wadau baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo wa siku mbili kuhusu matibabu kwa njia ya mtandao
Waziri wa mawasiliano sayansi na technologia mh MAKAME MBARAWA leoamezindua mkutano wa siku mbili wa wadau wa huduma ya matibabu kwa njia ya mtandao (TELEMEDICINE)  wenye lengo la kujadili jinsi ya kuboresha huduma hiyo pamoja na changamoto zake.

Akifungua mkutano huo waziri MBARAWA amesema kuwa huduma ya telemedicine ni muhimu sana kwa wananchhi wa Tanzania,kutokana na ukweli kuwa ni huduma ya haraka na isiyogharimu  kwenda umbali mrefu.


 

Huduma hiyo ambayo iliyofanyiwa  majaribio katika hospitali saba nchini imeonyesha mafanikio makubwa  na hivyo serikali inafikiria kuziunganisha  hospitali zote muhimu za wilaya na mikoa hapa nchini na huduma hiyo.
Akizungumzia jinsi huduma hiyo inavyofanya kazi waziri mbarawa amesema kuwa  ni huduma ambayo inatafutwa kama huduma nyingine isipikuwa utofauti wake ni huduma ambayo inapatikana  kwa haraka kutokana na kuhusisha mtandao.


Kwa mujibu wa huduma hiyo ni kwamba Daktari  anaweza kuwasiliana  na Daktari ambaye yupo hosipitali nyingine na kuweza kutoa maelekezo moja kwa moja kwa daktarri husika  kwa ajili ya kumhdumia mgonjwa na huuduma kuendelea kama kawaida.
Aidha katika hatua nyingine wizaya yake pamoja na wizara ya afya wamekubaliana na mtandao wa VODACOM TANZANIA kuanza kutoa huduma ya mtandao bure katika hospitali ya taifa muhimbili ikiwa ni jitihada za kurahisisha huduma katika hospitali hiyo
Wkifafanua kuhusu huduma hiyo inavyofanya kazi wataalam mbalimbali toka wizara ya afya na mawasiliano wamesema ni huduma ambao inafanywa kwa njia ya mitambo

"Mama yako mzazi yu mgonjwa mahututi katika hospitali ya Wilaya ya Masasi. Madaktari wamelifahamu tatizo lake lakini hakuna vifaa wala wataalamu wa jinsi ya kumtibu. Anatakiwa ahamishiwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako kuna madaktari bingwa na vifaatiba vya uhakika. Hata hivyo safari ya kutoka Masasi hadi Dar Es Salaam, pengine yaweza kupoteza uhai wake.
Lakini usihofu... Tanzania sasa imepata neema baada ya kuwepo kwa huduma ya Tiba kwa njia ya Teknolojia ya habari na mawasiliano, kwa kitaalamu ‘telemedicine’
 

Telemedicine ni utoaji wa huduma za afya au mbadilishano wa taarifa za kitiba kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano.*
*Mafanikio ya uvumbuzi huu yamesaidia  wataalamu wa afya kubaini na kutibu wagonjwa bila kuonana nao uso kwa uso.*
*Kwa kifupi, unaweza ukazungumza na daktari wako na kumweleza vile unavyojisikia, kisha akakuandikia vipimo, na baada ya kumpa majibu ya vipimo hayo kwa njia ya teknolojia pia, atakuandikia dawa au kukupa ushauri wa kitiba.

 Pia, Hospitali yenye vifaa na wataalamu wanaweza kuzungumza na madaktari katika hospitali za vijijini na kutoa ushauri wa jinsi ya kumtibu mgonjwa aliye taabani.
Hivi sasa hospitali saba nchini zimeunganishwa katika mradi  huo wa Telemedicine ambazo ni Mwananyamala, Amana, Temeke na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) pamoja na hospitali ya Tumbi, Mkoa wa Pwani.
Mei, 2011 ndiyo wakati ambao Rais Jakaya Kikwete alizindua  mradi huu akiwa pamoja na Makamu wa Rais wa India, Dk Manmohan Singh.
Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Modou Gaye anasema teknolojia hii inawezesha madaktari walioko katika Hospitali za Amana, Mwananyamala, Temeke, Tumbi na Bagamoyo kuwasiliana moja kwa moja na madaktari bingwa pamoja na watalaamu wengine walioko Muhimbili katika kujadili, kushauriana na
hatimaye kufanya uamuzi kuhusiana na tiba, uchunguzi wa mgonjwa husika.
 

Gaye anasema kuwa teknolojia hii itamwezesha mgonjwa aliyeko kati ya ospitali hizo kupata matibabu bila kufika Muhimbili.Anasema kupitia teknolojia hii wataalamu wataweza kuwasiliana katika nyanja za ushauri, vipimo vya uchunguzi mathalan vya radiolojia,  vipimo vya uchunguzi vya patholojia, magonjwa ya moyo na mafunzo kwa watalaamu.
Uwepo wa teknolojia hii utawezesha mgonjwa anayehitaji kupata huduma za kibingwa Muhimbili kutibiwa haraka na kwa muda mfupi kuliko ambayo angefuata utaratibu wa rufaa na hivyo kumpunguzia muda wa kukaa hospitalini kwa muda mrefu.

No comments