SAKATA LA MGOMO WA WAFANYABIASHARA---UMOJA WA WAFANYA BIASHARA WAWAVAA TRA SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
![]() |
Na Karoli
Vinsent
HUKU kukiwa bado wingu likiwa
limetanda kuhusu Hatma ya mgomo wa Wafanyabiashara wanaouza maduka maeneo ya
Kariakoo kutokana na mgomo huo kuzidi kuendelea,nao Umoja wa Wafanya Biashara
wadogo wadogo nchini umeibuka na kuivaa Mamlaka ya ukusanyaji kodi nchini TRA
na kusema ndio wanaosababisha Mgomo huo,
Kutokana na Mamlaka hiyo
kuanzisha mfumo mpya wa kukusanya kodi pasipokuwa kuwa na ujuzi wa mfumo
waliouanzisha.
“Kusema kweli mgomo huu,sisi umoja
wa wafanya biashara hatuhusiki kabisa kwani Tra ndio wanahusika kwa kitendo
chake cha kuanzisha mfumo mpya wa ukusanyaji kodi wa kietroniki ambao hawana ujuzi kabisa kwani
tufahamu kwamba Tanzania ni nchi ya kwanza Duniani kutumia mfumo huu wa
ukusanyaji kodi”
“ kwa
kutumia mashine za kietroniki ndio maana wanashindwa kutatua kero wanazozidai
wafanyabiashara wa maduka kuhusu mfumo huu kutoka na wao kushindwa hata pakwenda pakujifunza”alisema Minja
Minja alizidi
kusema kauli anayoitoa Mkurugenzi huduma ya mlipa kodo kutoka Tra,Richard Kayomba kuhusu mgomo huo sio kweli
kwani umoja huo hahusiki kwenye mgomo huo kwani Mamlaka hiyo ndio chanzo cha
mgomo huo kutokana na wao kuwafungia maduka wafanyabiashara hao,
Aidha Minja aliitaka mamlaka hiyo
kutatua changomoto zinazotokana na mfumo huo,kwani ndio chanzo cha matatizo.
Katika
hatua nyingine jumuiya hiyo ya wafayanya biashara imesema mkutano wao mkuu utafanyika tarehe 6 mwezi huu mkoni Dodoma
na kuwataka wafanya biashara watokeze kwa wingi ili kuja kujadili changamoto
zinazotokana na mfumo mpya wa ukusanyaji kodi na masuala mengine

No comments
Post a Comment