MWIGULU NCHEMBA AWATULIZA WAFANYABIASHARA NCHINI,JITIHADA ZAKE ZAMALIZA MGOMO RASMI SOMA HAPA KUJUA

Na Karoli
Vinsent
NAIBU Waziri
wa Fedha Mwigulu Nchemba ameitaka
Mamlaka ya mapato nchini (TRA)kusitisha mara moja mpango wake wa kuyafungia
Maduka ya wafanya biashara ndogondogo nchini,badala yake ameitaka Mamlaka hiyo
itatue changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao.
Hayo yalisemwa leo Jijini Dar es
Salaam na Mwenyikiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Johson Minja
wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari uliotishwa mahususi kwa ajili ya
kuzungumzia Mkutano mkuu wa Dharula uliitishwa na Wafanyabiashara nchi nzima,
uliofanyika Dodoma Mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Naibu Waziri
wa Fedha
Mwigulu Nchemba aliiwakilisha Serikili kwenye mkutano huo,
Ndipo katika Mkutano huo wafanyabiashra
walimuelezea Changamoto Mbalimbali zinazowakaili kuhusu mfumo mpya wa Mashine
ukusanyaji kodi ya Kitroniki EFD,
Baada ya
kuwasikiliza wafanyabiashara hao,Mwigulu nchemba aliwaamulu mara moja Mamlaka
ya Mapata nchini TRA kuacha kuyafungia maduka yasiyokuwa na Mashine za EFD .
“katika
mkutano na Mwigulu Nchemba kwa kuwa ndio mtu mwenye mamlaka ya juu kimaamuzi na
kumweleza changamoto zinazotukabili wafanya biashara na akutuelewa ndipo
akafikia maamuzi ya kuwaomba TRA waache kuyafungia maduka na kutatua
changamoto zinazowakabili wafanya biashara
kuhusu mfumo huu wa ukusanyaji kodi wa Mashine za EFD,”alisema Minja.
Minja alizidi
kusema Naibu waziri huyo aliendelea kutoa maamuzi mengine ikiwemo Kubadilisha Sheria ya Kodi ya
Ongezeko la thamini,VAT,kushughulikia ombi la kuwa na kipindi cha kufanya
biashara bila kulipa kodi kwa wafanyara wapya pamoja kwenda kupitia makabrasha
aliyokadhiwa yenye hadibu za rejea za vikao vya kamati na baadae atawaita kutoa
maamuzi,
2 comments
UMEPOTOSHA UMMA
Kimsingi wafanyabiashara tunasikitika mfumo wa efds kuangalia mauzo tu, wakati kuna gharama za manunuzi na za uendeshaji haziangaliwi hata kidogo, sasa unadhani hapo kuna fair
Post a Comment