EXCLUSIVE--SAMWEL SITTA AZIDI KUWAPUUZA MAASKOFU,AJIFANYA JEURI,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

Na Karoli
Vinsent
KILE kinachoonekana ni kuchoka kisiasa pia kuzeeka, kwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba,Samwel Sitta baada ya hivi sasa
kuwapuuza viongozi mbalimbali wa Dini waliomtaka kuacha kuzika maoni ya wananchi
yalitolewa kwenye Rasimu ya pili ya Katiba,Mtandao huu unaripoti.
Viongozi hao wa dini ya Kikristo
katika tamko lao walilitoa linasema Bunge maalum la katiba haliwezi kuleta
katiba Mpya badala yake litaishia kukwamisha matarajio ya wanananchi ya
upatikanaji wa Katiba.
Tamko hilo la Madhehebu hayo limetolewa
na Fungamano la Majukwaa Manne ambayo ni Christian Council of Tanzania (CCT),Tanzania
Episcopal Conference (TEC) The Council of Pentecostal Churches of Tanzania
(CCPCT) na The Seventh day Adventist,Tamko hilo lilisema wazi kwamba Bunge la
katiba alijadili Rasimu ya Katiba bali wanajadili Ilani ya Chama cha Mapinduzi
CCM,
Sitta ambaye ni Waziri wa Uhusiano wa
Afrika Mashariki, mara kwa mara amekuwa akiwabeza watu waliokuwa wakimshauri
kuhusu kulisitisha Bunge hilo ili kutafuta maridhiano ya Kisiasa lakini bado
mwenyekiti huyo anawaita watu hao ni Mbumbu wa hoja.
Machozi ya Viongozi hawa wa Dini
yamekwenda moja kwa moja, kwa mwenyekiti wa Bunge la katiba huyo na kusema
Sitta ameshindwa kusimamia Sheria ya iliyotungwa na Wajumbe wake na kwa kitendo
chake cha kusema Bunge hilo kwa kisingizio cha wajumbe wengi.
Tamko hilo la Maaskofu limeibua hoja
baada kugundulika kwamba Sitta amevunja Katiba sura ya 83 sheria ya Mabadiliko
ya katiba kwa kuzidi kupokea maoni ya wananchi ambapo sheria hiyo imekataza.
Lakini bado Mwenyekiti huyo anatumia
udikteta wake kupinga hoja za Viongozi wa dini hao wanaomtaka asikilize maoni
ya wananchi,
Sitta anazidi kuonekana kukosa usawa wa
Kisiasa baada ya Wiki iliyopita Bungeni alimbeza Mwandishi wa Habari Mwandamizi
na Mzalendo wa Nchi yake Saed Kubenea ambaye alikwenda kufungua kesi mahakamani
kushinikiza Bunge lisitishwa kwa madai halina uharali wa kisiasa,
Na kuzidi kusema mwandishi huyo anatumiwa,na kuzidi kujisifia
kwamba yeye ni mtu makini na asiyeyumbishwa na mtu na kusema yeye anasifa za
kugombani Urais ndani ya chama cha mapinduzi,
Akilizungumzia hili,Mjumbe wa
Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi NEC kutoka kwenye mikoa ya kusini ambaye
akutaka Jina lake litajwe kwenye Mtandao huu alisema anamshangaa sana Samwel
Sitta kwa kuchakaa kwake kimawazo kwa kitendo chake cha kupuuza mawazo ya
Viongozi wa Dini.
“Hiki ni
kichekesho sana ndugu yangu tena aingii akilini kabisa anachokifanya huyo mzee
sitta ni upuuzi kabisa leo ameanza kupokea maoni mapya wakati kazi hiyo
ilifanywa na tume ya Jaji warioba,sasa yeye naye anapokea maoni harafu chama
kinamwacha wala akimkemei tena,
“ kinamwacha
sasa huyo mtu ataleta machafuko tu akiaachiwa hivi na kama anajidanganya
atapewa Urais hana sifa hata ya kupewa tena hata ubunge aliokuwa nao”alisema
Mjumbe huyo
Rasimu
hiyo inayochkachuliwa na Sitta iliyowasilishwa na Jaji Joseph Warioba,
inapendekeza muundo wa muungano wa Shirikisho la Serikali tatu, lakini CCM
imeipindua na kurejesha muundo wa sasa wa Serikali mbili, licha ya kwamba Bunge
hilo bado halijafanya uamuzi wa kura kwa sura ya kwanza na ya sita zinazohusu
muundo wa muungano.
Katika taarifa hizo ambazo
zinaendelea kuwasilishwa na wenyeviti wa Kamati za Bunge hilo, maoni ya wajumbe
walio wengi yamefuta ibara nyingi za mapendekezo ya rasimu na kuingiza mpya,
kurekebisha zingine na kuingiza Sura mpya kuhusu masuala kadhaa ambayo Tume ya
Jaji Warioba iliyaacha yashugulikiwe na serikali za nchi washirika za Tanganyika
na Zanzibar.
Sura mpya zilizoingizwa ni
kuhusu Ardhi, Rasilimali na Mazingira, Serikali za Mitaa wakati suala la
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kamati zimetofautiana kwa
wajumbe wengine kutaka iingizwe katika Sura ya kumi na tatu ya rasimu inayohusu
Taasisi za Uwajibikaji
No comments
Post a Comment