GAZETI LA TANZANIA DAIMA LAZIDI KUBANWA NA SERIKALI,SASA UHAMIAJI WA CHACHAMAA,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
| Pichani ni Naibu kamishna wa Uhamiaji ambaye pia ni Msemaji Afande Abbas Irovya Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam, |
Na Karoli Vinsent
IDARA
ya Uhamiaji nchini imelitaka gazeti la Tanzania Daima kupelekea ushahidi wa
Madai ya Rushwa waliyoishutumu Idara hiyo.
Kauli
hiyo ya Uhamiaji nchini inakuja siku moja kupita baada ya Gazeti la Tanzania
Daima toleo la jumapili tarehe 7 mwezi huu lenye kichwa kikubwa cha Habari
“Ufisadi uhamiaji”
![]() |
| hili ni toleo liloandika habari yenyewe |
ambapo
toleo hilo lilisema viongozi wa idara ya uhamiaji wamepokea rushwa ya sh
milioni 2 kwa watu kila mtu aliyepewa ajira kwenye idara hiyo na kusema katika
watu 200 waliopewa ajira Idarani hapo walitoa pesa hizo ambapo jumla ya fedha
zote inafikia Bilioni 2.1
Akikanusha taarifa hiyo leo Jijini Dar Es Salaam Wakati wa Mkutano na
Waandishi wa Habari, Naibu kamishna wa Uhamiaji ambaye pia ni Msemaji Afande
Abbas Irovya,ambapo alisema Idara hiyo imesikitishwa sana na taarifa kwenye
gazeti hilo kwani taarifa hiyo inalengo la kupotosha Umma na kuichafua idara
hiyo nyeti ya nchi,kwani ukweli ni kwamba mwandishi wa Habari hiyo Martin
Malera ,alishindwa kuweka ushahidi wa moja kwa moja
“Habari kwenye Gazeti la Tanzania Daima toleo
la jumapili tarehe 7 mwaka huu imetusikitisha sana kwani habari haina ukweli
wowote tena inamalengo ya kutuchafua tu,kwasababu mwandishi wa habari hiyo
ameshindwa kuweka hata ushahidi wa moja kwa moja juu ya hao vigogo anaosema
kwamba wamechukua rushwa ya Bilioni 2.1 zaidi ya kusema ni kwa mujibu ya vyanzo
vyetu,tena mbaya zaidi ameshindwa hata kutufwata sisi watu wa uhamiaji ili
kupata ukweli yeye kaishia kuandika Habari ambayo haina ukweli “alisema Irovya
I rovya alizidi kusema idara hiyo inamtaka mwandishi wa Gazeti hilo
apeleke Majina ya hao vigogo wa uhamiaji ambao anaowashutumu ili idara hiyo
iwachukulie hatua kali za kisheria kwani kufanya hivyo kutaweza kuijenga idara
hiyo kwa Wananchi,
Aidha Irovya aliwataka Waandishi wa Habari nchini kufanya kazi kwa kuzingatia
Weledi mkubwa sana ili taarifa zao ziweze kuleta manufaa kwa jamii,
Huu ni Mwendelezo wa kuzidi
kubanwa kwa Gazeti la Tanzania Daima ikumbukwe karipio hili la Idara ya
Uhamiaji limekuja siku chache kupita baada ya Ofisi ya Msajili wa Magazeti
nchini kuliandikia barua gazeti hilo na kusema liache kuandika habari zenye
upotofu kutokana na moja ya matoleo yake yaliyopita,
yenye kichwa cha Habari “Rais
Kikwete ayalamba Matapishi yake” pamoja na “Rais Kikwete anywea” Kwa mujibu ya
Barua hiyo ililitaka Gazeti hilo kukanusha taarifa kutokana na habari hiyo
Kukwaza Rais Jakaya Kikwete, Baada Barua hiyo kulifikia Gazeti hili,ndipo
Mhariri wa Gazeti hilo katika toleo la leo tarehe 9 mwezi huu,Katika ukurasa
wake wa Kwanza lilikuwa na Kichwa cha Habari “Kumradhi Jakaya Kikwete

No comments
Post a Comment