Zinazobamba

EXCLUSIVE--WAZIRI NYALANDU AJIBU MAPIGO YA MAGAZETI,AIBUKA NA KUSEMA MAZITO SOMA HAPA KUJUA

Pichani Ni Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu
Na Karoli Vinsent
BAADA ya kushutumiwa na magazeti mbalimbali nchini kwa kuzidisha vitendo vya Ujangili nchini Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu ameibuka na kusema yote yanayosemwa juu yake hayana ukweli bali yanalengo ya kumzorotesha katika Ufanisi wake wa kazi,
                Kauli hiyo ya Nyalandu ameitoa huku kukiwa bado kuna taarifa zinazoenezwa na magazeti mbalimbali nchini kwamba Waziri huyo ameshinikiza kutolea kwa kibali kutoka Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete kwenda kwa Marafiki zake kutoka Kimarekani  ili waweze kuua tembo pamoja na wanyama wengine 704,

                  Waziri Nyalandu alitoa Masikitiko yake Leo Jijini Dar Es Salaam wakati alipokuwa anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu mara baada ya kumalizika mkutano uliowashirikisha Viongozi mbalimbali kutoka duniani na kuwepo na  mwakilishi wa Benki ya Dunia hapa nchini  na Viongozi mbalimbali wa kisiasa ,mkutano huo wenye lengo la kupambana na Vitendo vya Ujangili nchini,
             Ambapo Waziri Nyalandu alipoulizwa na Mwandishi wa Mtandao huu juu ya Taarifa zinazoenezwa na Magazeti mbalimbali juu ya yeye kushinikiza kutolewa kibali kutoka Ikulu kwenda kwa Familia ya marekani ambao ni Marafiki zake ndipo Nyalandu alisema anasikitishwa sana na Taaifa hiyo na kusema taarifa hiyo haina ukweli inazusha na Magazeti kutokana na magazeti hayo kutumiwa na Majangili.
            “Kiukweli taaifa hiyo haina ukweli kabisa tena kibali ambacho anakisema Magazeti hayo, Ikulu haina uwezo wa kutoka kibali kwa Mambo hayo,kwanza hata mimi nashangaa sana na siwezi kushindana nao naacha tu kwasababu wanajua msukumo wao wa kuandika habari hizo”alisema Nyalandu.
           Nyalandu alizidi kusema kwa sasa anawaomba Watanzania waamini ufanyaji wake kazi katika Wizara hiyo ya Maliasili kwani unalengo la kupambana na Vitendo vya Ujangili nchini,
           Katika hatua nyingine Waziri Nyalandu alizungumzia Ajenda mbalimbali walizozungumzia katika mkutano huo uliowashirikisha mataifa mbalimbali nchini na kusema kwa sasa vita ya Ujangili inazidi kupamba moto kutokana na kuzidi kusapotiwa na Mataifa mbalimbali Duniani na kuwataka Majangili popote walipo nchini watafute kazi zengine za kufanya na kuacha kazi ya kuua wanyama ambao ni Hazina ya Taifa.

      Naye Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mchungaji Peter Msigwa alisema mkutano huo umelenga kuonyesha njia mbalimbali katika kupambana na vitendo vya Ujangili nchini na kuwataka wananchi waache kusikiliza Taarifa zinazoandikwa na Magazeti zenye lengo ya kupotosha ukweli kwa Watanzania, 

No comments