Zinazobamba

HABARI NZITO LEO--SAMWEL SITTA YAMKUTA MAKUBWA,JUKWAA LA KATIBA LASEMA MAZITO KUHUSU YEYE SOMA HAPA KUJUA

Na Karoli Vinsent
       UDIKTETA,ubabe pamoja na chuki kwa watanzania anazofanya mwenyekiti wa Bunge Maalum La Katiba Samwel Sitta ndani ya Bunge hilo  kutokana na yeye kuhusika kwa kiasi kikubwa kuzika maoni ya Wananchi yaliyotolewa kwenye Rasimu ya pili, sasa yaanza kumkuta makubwa mwenyekiti huyo,
       Kutokana na Jukwaa la Katiba nchini (JUKATA) kuibuka na kusema watahakikisha kwenye uchaguzi mkuu mwakani 2015 kumwondoa kwenye nafasi alizo nazo,
            Nafasi hizo ni Ubunge wa jimbo la urambo Mashariki pamoja  sehemu zengine atakazogombania,
          Kauli hiyo kali imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba nchini (JUKATA) Deus M Kibamba wakati wa Mkutano na Waandishi Habari ambapo alisema wamefikia maamuzi hayo kutokana na kubaini kuwa mwenyekiti huyo kuhusika kwa kiasi kikubwa kuhujumu mchakato wa upatikani katiba mpya .

          “Huyo samwel Sitta ni Adui wa kwanza ambaye tumebaini kwamba anafanya makusudi kuhujumu katiba, huku akijua katiba ni maridhiano tena anadanganya umma na kusema thelusi 2 inapatikana kumbe haipatikana tena kibaya zaidi ameanza kupokea maoni kutoka kwenye makundi tofauti huku akijua wazi kazi hiyo ilishafanywa na tume iliyoundwa”
        “Tumeamua sasa tutashirikiana na Wananchi wa jimbo la Urambo kuhakisha Sitta hapewi  tena nafasi ya Ubunge aliyonayo kama akigombea tena kwenye uchaguzi mkuu 2015, aliyokuwa nayo hata pia udiwani akigombea asipewa”alisema Kibamba.
                 Kibamba alizidi kusema Mwenyekiti huyo wa Bunge la katiba amekuwa akifanya upotoshaji mkubwa kwa Watanzania kwa kitendo chake cha kusema wakati wa kupiga kura kwenye bunge hilo endapo mjumbe atakuwa nje ya nchi Basi atapigiwa simu na kutajiwa vipengele kwa njia simu na kupiga kura ndio au hapana.
            “Huu ni upotoshwaji mkubwa anaofanya Samwel Sitta na wakupingwa na kila mtu hivi anavyosema eti wakati wa kupiga kura  kwa Wajumbe ndani ya Bunge hilo kama mjumbe yupo nje ya nchi basi atapigiwa simu atatajiwa kipingele na yeye ataamua ndio au hapana,jamani huu ni zaidi ya upotoshwaji na sisi Jukwaa la katiba hatuwezi kukubali”alizidi kusema Kibamba.
            Katika Hatua nyingIne Jukwaa hilo la Katiba nchini limepongeza uamuzi uliofikiwa kati ya Rais jakaya Kikwete na Vyama vya kisiasa nchini vilivyo chini ya kituoa cha Demokrasia Tanzania (TCD) juu ya kulisitisha Bunge Maalum la Katiba na kusema maamuzi hayo ni mazuri yanahaja ya kupongezwa,
              Aidha Jukwaa hilo la katiba limetoa Wiki mbili tu kwa mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Bunge hilo la katiba kulisitisha mara moja Bunge hilo na sio octobar 4 kwani kuendelea na vikao hivyo ni kufanya wizi kwa Watanzania kwani Vikao hivyo haviwezi kuleta katiba mpya.
         Vilevile Jukwaa hilo limesema mwenyekiti wa Bunge hilo asipolisitisha,basi watashirikiana na wananchi nchi nzima kwenda mpaka mkoani Dodoma.

               “Tumetoa wiki mbili tu kwa mwenyekiti wa Bunge maalum pamoja na wajumbe wawe wameshaondoka na bunge lisitishwe na endapo endapo wakikaidi na kuendelea na vikao vya bunge basi,sisi Jukwaa tutashirikiana na watanzania kwenda mpaka Dodoma huku tukiwa tumeshika makufugi na kulifunga bunge hilo kwani hatutaweza kukubaliana na hujuma hizo,”alisema Kibamba. 

Hakuna maoni