HABARI NZITO LEO--UKAWA WAMVAA RAIS KIKWETE TENA,WAIBUKA NA WASEMA MAZITO SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
UKAWA |
Na Karoli Vinsent
SIKU moja kupita baada ya Rais Jakaya
Kikwete kufikia Maazimio na Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA kulisitisha bunge Maalum la katiba na kupisha
Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 ili kutoa mwanya wa kuifanyia marekebisho ya 15 ya
katiba iliyopo ya Mwaka 1977,
Nao Umoja huo wa kutetea Katiba ya Wananchi
UKAWA umeibuka na kumvaa Rais Jakaya Kikwete na kumtaka asitishe Bunge hilo
mara moja na kuacha mpango wake wa kulisitisha Bunge hilo Octoba 4,kwani
kufanya hivyo ni kupoteza pesa za Watanzania bure kutokana Vikao hivyo
vinavyoendelea haviwezi kuleta katiba bali vinaendelea kuteketeza pesa za
Wananchi,
Hayo yamesemwa leo jijini Dar Es
Salaam na Viongozi mbalimbali wa kisiasa wanaunda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi
UKAWA,wakati wa Mkutano na Waandishi Habari, mkutano huo wenye Lengo la
kujadili maazimio kati ya viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),na Rais Jakaya kikwete
uliomalizika Juzi Ikulu ndogo mjini Dodoma.
Ambapo
naye katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Mandeleo Chadema Dk Wilbroad Slaa
amesema anamshangaa sana Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa na huruma kwa
watanzania kwa kuzidi kuliruhusu Bunge hilo kuendelea hadi Oktoba 4 mwaka huu, kwani
huko ni kupoteza pesa za watanzania kutokana na
yeye Rais Kikwete wakati wa mkutano na Vyama vya hivyo vya Kisiasa alikibuliana
nao kwamba Mwenendo wa Bunge hilo hauwezi kuleta Katiba Mpya,
“Mimi namshangaa
jinsi Rais Kikwete anavyokubalia pesa za Watanzania zipotee bure kiasi hichi
pasipo kuwa na Sababu maana leo hii mpaka octoba 4 ni siku ishirini na ukipiga
hesabu za Wajumbe wote waliokuwa Bungeni kwenye Vikao vya Bunge garama yake ya
posho ni zaidi ya Bilioni 3.5 hurafu yeye mwenyewe Kikwete anakubali wazi
katiba haitopatikana sasa, huku ni kuchezea pesa za wananchi kabisa maana
ukweli huko wazi kabisa ndio maana tunamtaka sisi UKAWA alisitishe sasa bunge
hilo ili fedha hizo ziende katika mambo mengine yenye tija”alisema Dokta Slaa,
Dokta Slaa alizidi kusema
anamshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kutokuwa na huruma za watanzania kwani
anakubalina na watu mia sita kutoka kwenye bunge hilo laa Bunge la katiba na kuwapuuza watanzania
Zaidi ya Milioni 40 ambao hata mlo moja kwa siku ni kazi.
“Huyo ni Rais gani huyo
ambaye anashindwa hata kuwaonea huruma watazania wanaoteseka tena hata kula mlo moja kwa siku ni kazi,yeye anakubaliana na
wajumbe mia sita kuteketeza pesa za Wananchi,hivi kweli ndio kiongozi huyu,kwasababu
kiongozi makini ni yule anayeangalia Fedha za Chache kwa ajili ya manufaa kwa
wananchi wake”alizidi kusema Dokta Slaa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha
NCCR mageuzi James Mbatia alisema wao Ukawa wamepokea kwa moyo wote maamuzi
waliyofikia ya kuifanyia marekebisho ya katiba iliyopo na kusema Bunge la
katiba litakapohalishwa basi wakubaliane kamaandishi ili Rais
ajaye basi aendelee na mchakato huu asiupuuze,
“Sisi ukawa tunakubalina na kwa moyo
wate maanuzi tulitofikia katika mkutano na Rais Kikwete,na tunasema wazi tumekubaliana
kuhailisha mchakato huu basi tunataka tukubaliane kimaandishi kabisa ili Rais
ajaye baada ya Uchaguzi wa Mwaka 2015 aendelee na mchakato huu atutaki kabisa
kusikia eti Rais anayekuja ahamue kwa maamuzi yake hatutati kusikia ujinga huo”alisema
Mbatia
Mbatia ambaye naye ni Mjumbe wa Bunge
hilo Maalum la katiba aliongeza kusema wao Ukawa wamefikia uamuzi kwamba endapo
Bunge hilo la katiba litakapoendelea baada ya uchaguzi mkuu hawatakubali
kuongozwa na mwenyekiti wa sasa ambaye anaongoza Samwel Sitta na kuzidi kusema Mwenyekiti huyo hana sifa ya kuliongoza bunge
hilo kutokana na kuendesha siasa za chuki na ubaguzi.
Vilevile naye Mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba alisema wanamuomba Mkaguzi mkuu wa Hesabu
za Serikali kulikagua Bunge hilo la Katiba kwa madai bunge hilo lilitawaliwa na
Ufisadi wa kutisha kutokana mipango yake hiyo.
“Kiukweli namuomba Mkaguzi Mkuu wa
Serika alifanyie ukaguzi wa kimahesabu bunge hilo la katiba kutokana na Vikao
vyake hivyo kutawaliwa na ufisadi wa kutisha tumeona leo Jinsi kila mjumbe
mmoja kwa siku ametengewa bajeti ya chai ya shilingi Eflu kumi kwa siku tena chai ya asubuhi na jioni na hata
vipaza sauti pia, vyote hivi ni matokeo ya Ufisadi ndio maana tunamtaka
alifanyie ukaguzi wa kimahesabu”alisema profesa Lipumba.
Kuhusu kama Endapo Rais Jakaya asipofanyia
merekebisho katiba iliyopo?
Mwenyekiti
wa Chama cha NCCR mageuzi James Mbatia alisema endepo kama Rais Kikwete asipofanyia
marekebisho katiba iliyopo basi atakuwa amefanya usaliti kubwa na ajue ataliweka taifa kwenye machafuko makubwa
sana kwani Umoja huo hautokubaliana na yeye.
Katika Hatua nyingene Umoja
huo wa Katiba wa UKAWA umeitaka tume ya Uchaguzi nchini ilifanyie marekebisho
ya haraka Daftari la kudumu la wapiga kura ili liweze kuwaandikisha watanzania
ambao hawajapata Fursa hiyo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni