TGNP WAWAFUNDA WASANII WA KITANZANIA,WAWATAKA WASANII HAO KUTUMIA WASIFU WAO KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Msanii anayefanya vema kwa sasa Nasbu Abdul katika moja ya pozi lake maalufu, wasanii wa kitanzania wameshauriwa kutumia ngazi zao kukomesha mfumo dume
WASANII
wametakiwa kutumia nafasi wanazopata kupanda majukwaani kukemea vitendo
vya ukatili wa kijinsia na kudai uwajibikaji na upatikanaji wa huduma
za kijamii .
Akizungumza
na wasanii walioshiriki warsha ya siku moja ya TGNP iliyolenga
kuwajengea uwezo wasanii kutumia nafasi yao katika kudai uwajibikaji,
uandaaji wa bajeti kwa mrengo wa kijinsia na mapambano dhidi ya ukatili
wa kijinsia jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP
Mtandao, Lilian Liundi amesema kuwa wanasanii wana nafasi kubwa ya
kutoa elimu, kuburudisha, kuonya na kukemea na kuleta mabadiliko
chanya.
Amewataka
kutumia ipasavyo fursa walio nayo kuhakikisha wanapata uelewa wa
masuala yanayowagusa wananchi na kuandaa kazi zitakazosaidia kuleta
mabadiliko, kama filamu, Michezo ya majukwaani, mashairi, ngoma, na
uchoraji wa vibonzo.
“TGNP
Mtandao tunafanya kazi na vyombo vya habari kwa muda mrefu, wasanii
tunawatambua kama watoa taarifa pia, na mtindo wao wa utoaji wa taarifa
ni wa haraka na unapendwa na wengi, ndio manaa tunakutana na wasanii
kwaajili ya kuwawezesha kutumia fursa walizo nazo kupaaza sauti juu ya
changamoto za kijamii”alisema Liundi
Alisema
kuwa kila msanii ana hadhira yake na kama atakuwa na uelewa juu ya
masuala ya bajeti kwa mrengo wa kijinsia, akijua masuala muhimu
yanauyohusu mgawanyo sawa wa rasilimali hasa kwa makundi yaliyoko
pembezoni, akajengewa uwezo wa kufanya uchambuzi wa majukumu ya kijinsia
na mahitaji muhimu lazima jamii itabadilika na watendaji au watunga
sera nao watapata ujumbe na kuleta mabadiliko.
Kwa
upande wake Mwanachama na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP
Mtandao Usu Mallya, alisema kuwa Utandawazi na soko huria ambavyo
vimeingia kuanzia miaka ya 1990 vimeipelekea serikali kupunguza wajibu
wake wa kusimamia uchumi, ajira, masoko na biashara, sekta binafsi
imepewa majukumu makubwa zaidi ya kuwa injini ya kutafuta biashara na
masoko na kupelekea kuongezeka kwa tabaka na wanawake wamezsidi kubaki
nyuma kiuchumi.
“
Tunahitaji sana nguvu ya wasanii katika kuelimisha jamii na kushinikiza
mabadiliko. Mwanamke kujitoa kwenye umasikini ni kazi ngumu sana,
pamoja na majukumu aliyo nayo lakini bado hana maamuzi kuhusu fedha za
kutekeleza majukumu aliyo nayo”alisema Usu
Kwa
upande wake Stara Thomas, mwimbaji wa siku nyingi alisema kuwa katika
semina hiyo amepata mamabo makubwa ikiwa ni pamoja na kuuelewa mfumo
dume ni kitu gani na jinsi unavyoadhiri maendeleo ya jamii hasa wanawake
na watoto.
“katika
semina hii nimejifunza kitu kikubwa, nimeelewa maana ya mfumo dume na
jinsi unavyoadhiri jamii, nitatumia elimu hii katika kazi zangu za
sanaa ili kuleta mabadiliko”alisema Thomas
Naye
Mwimbaji Irene Sanga, alisema kuwa wasanii wanatakiwa kuitumia nafasi
waliyo nayo kuandaa kazi ambazo zitafikisha ujumbe wa kuleta
mabadiliko sio mapenzi pekee. “sisi tuna nguvu tunaweza kuleta
mabadiliko, bila wasanii hakuna sherehe wala misiba, tunauwezo mkubwa
wa kujibadilisha na kubeba uhusika wa kila aina tutumie vizuri fursa
hizi.
Mwisho
No comments
Post a Comment