EXCLUSIVE---MCHAKATO WA KATIBA MPYA WAANZA KUMCHAFUA RAIS KIKWETE KIMATAIFA,UJUE KWANINI SOMA HAPA KUJUA
pichani ni Rais Jakaya Kikwete picha na Maktba
Na Karoli
Vinsent
RAIS Jakaya
Kikwete uwenda akachafuka Kisiasa kwenye Medani za Kimataifa endapo mchakato wa
upatikanaji wa katiba mpya ukikamilika na katiba mpya kupatikana , bila ya kuwepo
wajumbe wanaounda umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA),umetajwa ndio itakuwa sababu itakayamshusha hadhi Rais
Jakaya Kikwete kwenye Medani za Kimataifa,Mtandao huu umebaini.
Rais Kikwete,ambaye hivi karibuni
ambaye amepewa tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo aliyopewa ya Nyota wa Demokrasia Afrika 2014-Icon of Demokrasia Award winner
for 2014 in Africa,
Tuzo hiyo aliopewa na jarida la the
Voice kutokana na michango mbalimbali ya kidemokrasia aliyoionyesha barani
humu,ikiwemo jitihada alizozifanya za kutuliza amani nchini Kenya kwenye
machafuko ya Kisiasa mwaka 2007,ambapo Rais Kikwete alifanikiwa kutuliza amani
nchini Humo.
Lakini kwa sasa Rais Kikwete
ameanza kuchafuka kisiasa kimataifa kwa kitendo chake cha kuharibu mchakato wa
upatikanaji katiba mpya,
Kwa mujibu ya taarifa mbalimbali
kutoka kwa mataifa tofauti Duniani zinasema macho na masikio kwenye mataifa
mengi yameelekezewa Tanzania katika
kipindi hiki cha Historia cha undikaji wa Katiba ambayo sasa imekuwa na mpasuka
mkubwa ambao umesababishwa na Ghiliba za chama chaMapinduzi CCM,kwa kuyapuuzia
maoni ya wananchi na kuanza kuingiaza maoni ya chama hicho.
Na endapo Rais Kikwete ataungana na
mafahidhina kutoka chama chake ambao hawapendi upatikanaji wa Katiba mpya na
kuzidi kuendelea kushikili bango suala la Serikali mbili na kuyachingia mbali
maoni ya Serikali tatu ambayo yaliyotolewa na wananchi kutazidi kushusha umaharufu wake Kisiasa alioanza kuupata
Duniani licha ya yeye kushidwa kuondoa Umasikini.
Kwa upande wake akilizungumzia hili,
Mwanasheria wa Umoja wa Kutetea katiba ya Wananchi UKAWA,Tundu Lissu amesema
kwa hali ilivyo basi ni ishara tosha hakuna uharali kuhuhu tuzo anazopewa Rais
Kikwete.
“Ngoja niseme Mataifa makubwa
Yanayotunyonya yanatumia mahusiano na Vibaraka kwenye nchi husika ambazo wanaziibia Fedha kupita uwekezaji kama
madini pamoja na Mabenki yao yaliyokuwepo nchini,na wanakuja kutoa shukrani kwa
kuwapa Tuzo na kwa hali hii mimi sioni Jipya juu yeye kuchafuka kwenye madeni
za kimataifa”alisema Lissu.
Tundu Lissu ambaye ni Mjumbe pia wa Bunge
Maalum la Katiba alizidi kushikilia bango kwamba wao hawatarudi kwenye Bunge
hilo Maalum la katiba kutokana na leo kuanza kujionyesha wazi kwamba
wanaendeleza mambo yao.
“Umeona mwenyewe leo wameanza
kubadilisha kanuni na wanafanya hivi iliwaendeleze kutunga katiba itakayotokana
na Maoni ya chama cha CCM na kuzika maoni ya Wananchi na tunasema sisi
hatutoshiriki kwenye jambo hili na hatuwezi kurudu”aliongeza Lissu
Akizungumzia na Mtandao huu pia,
Mchambuzi wa Masula ya Kisiasa kutoka chuo kikuu cha Dodoma Nchini, Seiph
Yahaya alisema huu ni wakati wa kumpima kisiasa Rais Kikwete kuhusu uharali wa
tuzo anazopewa je zina stahili?
“Na sasa ni wakati mzuri sana
wa kupima Rais jakaya Kikwete kwenye huu
mchakato wa katiba Maana mchakato huu wa katiba ukiendelea hivi pasipo kuwa na
upande mmoja wa kisiasa ambao ni UKAWA unaweza kumchafua sana Rais Kikwete kimataifa
kwani inaonekana kwa zile Tuzo alizopewa ni za kiupendeleo”alisema Yahaya
Yahaya aliongeza na kusema kama Rais
aliweze kutuliza Amani nchini Kenya anashindwa vipi kuachana na Ghiliba za
chama chake ambazo wanashikilia mfumo wa Serikali mbili ambao utokani na Maoni
ya wananchi na kuuacha mfumo wa Serikali tatu uanotokana na Maoni ya Wananchi.
Mchakato
huo
wa upatikanaji katiba mpya ambao teyali umeanza kuingia dosari kwa
kitendo cha Baadhi wajumbe wanaounda Umoja wa katiba ya Wananchi UKAWA kususa
vikao hivyo vya Bunge Maalum la Katiba kwa madai ya mchakato huo Kuhujumiwa na
chama cha Mapinduzi CCM.
Licha umoja huo kususia Vikao hivyo vya Bunge Viliovyoanza
leo Mkoani Dodoma bila ya kuwepo ,Lakini Bado chama cha Mapinduzi
CCM,kimepuudha madai hayo ya ukawa na kuendelea na kazi ya kujadili Rasimu ya
pili iliyowasilishwa na Tume ya ukusanyaji wa Maoni.
Umoja huo wa UKAWA ni muunganiko wa
Vyama vya kisiasa ikiwemo, CUF, DP na NCCR-Mageuzi vilivyosusia
na kutoka nje ya Bunge,pamoja na wajumbe 201 waliochaguliwa na Rais,
Lakini Vikao hivyo
vya Bunge la katiba vimeanza leo bila ya kuwepo UKAWA,ambapo Mwenyekiti wa
Bunge hilo Samweli Sitta alijinadi na kusema wananchi wategemee kupata katiba
bora yenye kuwaletetea Maendeleo.
Sitta,ambaye pia ni
Waziri wa Uhusiano wa Afrika Mashariki alisema hata kama upande mmoja ya
wanaojiita UKAWA kutokuwepo Bungeni haitazuia wao kutotengeneza katiba.
Duru za mbalimbali za
Kisiasa zinasema kauli hizo za Samwel Sitta zinaweza kuvuruga Amani ya nchi
kutokana na yeye kushindwa kujua kwamba Katiba inatokana na Maridhiano,ambaye
Waziri Sitta anapuuzia suala hilo.
No comments
Post a Comment