HABARI NJEMA--WIZARA YA SAYANSI YATOA NEEMA VYUO VIKUU NCHINI SASA YAZINDUA MRADI BOMBA---SOMA HAPA KUJUA MRADI GANI HUO
Hapo ni Sehemu ya uzinduzi wamradi wa
mtandao wa Intaneti unaounganisha takribani vyuo vya elimu ya Juu na Taasisi za
Utafiti zipatazo 28.
Na Karoli Vinsent
WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
Makame Mbarawa amewataka wanafunzi na walimu wa vyuo vikuu nchini kuhakikisha
wanatumia mitandao ya kijamii kwa maslahi ya taifa.
Kauli hiyo inatokana na matumizi
mabaya ya mitandao kwa baadhi ya wanafunzi, walimu na watu mbalimbali, hali
inayochangia kuporomoka kwa maadili na kuongezeka kwa matukio ya uhalifu.
Rai hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam leo, wakati akizindua mradi wa
mtandao wa Intaneti unaounganisha takribani vyuo vya elimu ya Juu na Taasisi za
Utafiti zipatazo 28.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Tanzania Daima Mika Ndamba akiuliza swali kwenye uzinduzi huo
Mbarawa alisema, mitandao ya
kijamii inauwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko ya kimaendeleo hasa kupitia
ushawishi waliokuwa nao wanafunzi na walimu katika kuibadilisha jamii kuwa na
mtazamo chanya juu ya mitandao hiyo.
Alisema, miongoni mwa hasara
zinazoweza kuwapata wanafunzi juu ya matumizi mabaya ya mitandao hiyo ni
kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
“Naamini jamii itabadilika, kwani
kuna sheria tatu ambazo zimetungwa ili kudhibiti matumizi mabaya kama Sheria ya
matumizi ya Kompyuta, biashara na uhifadhi wa kumbukumbu katika kompyuta ambazo
zote tunatarajia kuzipeleka Bungeni ili zipitishwe na kusimamia matumizi sahihi
yenye tija kwa taifa” alisema Mbarawa.
Hata hivyo alitumia fursa hiyo
kuzungumzia mradi aliouzindua kuwa unalenga kuongeza idadi ya wahitimu wa vyuo
vya juu wenye sifa stahiki katika maeneo ya Sayansi, Teknolojia, Elimu na
Utawala kupitia mazingira ya kujifunza yaliyoboreshwa.
“Mradi huu umegharimu sh. bilion 4.6,
ambao tulipendekeza kwenye maeneo manne kama Kukuza uchumi, kujenga uwezo wa
Kuandaa Walimu watakaofundisha vyuo vikuu, kujenga uwezo wa taasisi maalum za
elimu ya juu na uwekezaji wa TEKNOHAMA katika Sekta ya Elimu” alisema.
Aliongeza kuwa, Wizara ya
Mawasiliano inasimamia utekelezaji wa eneo la uwekezaji wa TEKNOHAMA
inayounganisha Vyuo vya Elimu ya Juu na Taasisi za Utafiti ili kuongeza huduma
za Maktaba kwa kutumia Elektroniki pamoja na Mfumo wa Kuhifadhi kumbukumbu za
Elimu.
No comments
Post a Comment