NI BIFU KATI CLAUDS FM NA UKAWA--TUNDU LISSU AIBUKA AWAVAA NA ASEMA MAZITO,SOMA HAPA KUJUA ALICHOKISEMA
Pichani ni mwanasheria wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA Tundu Lissu pamoja mch Peter Msigwa
Pichani ni Mkurugenzi wa Clauds Media Group Joseph Kusaga picha na maktaba
Na Karoli Vinsent
SAA chache
kupita Baada Radio ya Clauds Fm kutangaza Rasmi kutozisoma Habari zozote zinazowahusu Wajumbe wanaunda
umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA,
kwa kile wananachodai Umoja huo hauna jipya bali unataka umaharufu tu.
Kauli hiyo ya ambayo inakwenda
kinyume na Maadili ya Vyombo vya Habari imetolewa leo na Mtangazaji wa Kipindi
cha Power breakfast Babla hassani wakati wakichambua magazeti ya siku ambapo
alisema kwa sasa hawatazisomi habari
zozote zinazohusu umoja huo wa Ukawa kwa madai umoja huo ni wabinafsi na hawana
jipya bali wanataka Umaharufu.
Naye Mwanasheria wa Umoja wa kutetea
katiba ya Wananchi UKAWA ,Tundu Lissu amewavaa na kusema Radio hiyo inajimaliza na ndio itakuwa inaonekana wazi
inapendelea Upande moja Kisiasa.
Kauli hiyo Tundu Lissu,ameitoa mda huu wakati
alipokuwa anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu,Kuhusu wao Ukawa wamepokeaje Taarifa hiyo ya kutosomwa
Habari zao kwenye Radio hiyo.Ambapo Lissu alisema hizo taarifa anazisikia na
kama ni kweli wametangaza hivyo watakuwa wamejimaliza.
“Kwanza nimezisikia hizo taarifa na
kama kweli aliyosema huyo mtangazaji ndio msimamo wa Radio nzima basi watakuwa
watu wa Ajabu sana maana leo Nchi nzima habari ya Mjini ni Ukawa,leo utasemaje
ukawa ni wabinafsi wakati wasomi na watu wengine wanaungana na sisi leo
inakuwaje Radio hiyo iseme hivyo kama wako upande mmoja wa Kisiasa weseme”alisema
Lissu.
Tundu Lissu,ambaye naye ni Mjumbe
wa Bunge maalum la Katiba alizidi kusema yeye sio mwanahabari bali anachokijua
huo utakuwa msimamo wa Radio nzima na wao Ukawa hawata ogopa na kuacha kuwatetea
wananchi kwani wako kwa ajili ya kuwakomboa wananchi na hawezi kukatishwa na tamaa
na watu wachache wenye maslai ya upande mmoja.
“Harafu inashangaza sana leo nchi
nzima inazungumzia Ukawa harafu mtua aseme leo Ukawa utotangaza habari zao kwa misingi hipi?”alihoji
Tundu lissu.
Kauli hiyo ya Tundu
Lissu,imetolewa saa chache kupita baada Mtangazaji wa kipindi cha Power
Breakfast Babla Hassani,kutangaza Rasmi kwamba hawatasoma Habari zozote
zinazohusu Umoja huo.
“Mimi Naona kusoma Story zinahusu
Ukawa tunawapa kiki tu wao siwamekuwa kutupotezea kutorejea Bunge I whon doing,vile
vikao vinawanufaisha watanzania wote wao ni wabinafsi tu,the best ican do
tuwapotezea Habari zao, na ukiona habari inahusu Ukawa tu usisome hapa kwenye
Redio,na wakae huko nje atuwataki Ukawa bungeni”alisema
Babla Hassani.
Kauli hiyo ya iliungwa Mkono pia na Mtangazaji wa mwengine wa kipindi hicho,
Paul Jems anayejulikana kwa jina la Umaharufu “PJ” naye alisema kwanzia sasa
hatazisoma habari zozote zinazohusu Umoja huo kwani wanapoteza pesa za wananchi
bure kwa kususia bunge hilo.
Msimamo huo wa Watangazaji hao unakwenda
Kinyume na Mmiliki wa Radio hiyo ya Clauds Fm Joseph Kusaga alipokuwa anahojiwa
na kipindi kimoja cha runinga kutoka nchini Uingereza kinachojulikana,The
Sporah Show ambapo katika kipindi hiko alisema Radio yake haina upande wowote wa Kisiasa
na kuongeza ni Redio huru inayofanya kazi bila kushabikia upande wowote.
Lakini kwa sasa kauli ya Mmiliki
hiyo inakwenda tofauti na ilivyo,na kama Radio ikifanya kama inavyofanya hivyo
kwa sasa,Basi Redio hiyo itapelekea machafuko makubwa kama yaliyowai kutokea
nchini Rwanda na kuua maelfu ya watu,na sababu kubwa ni Radio za nchini humu
zilikuwa na misimamo kama walioyonayo Clauds.
Umoja huo wanaupinga wa Ukawa unaundwa na Muunganiko wa Vyama vikuu
vya Upinzani ikiwemo Chama cha
demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Chama cha wananchi CUF,Chama cha Mageuzi
NCCR,ND pamoja na Baadhi ya wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Kikwet e.
Umoja huo umegoma kurejea kwenye Vikao vya
Bunge la katiba kwa madai rasimu inayotokana na Maoni ya wananchi
kuchakachuliwa,na kitendo hicho cha Ukawa kimeungwa mkono na wananchi
mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Dini pamoja wajumbe wa iliyokuwa tume ya Jaji
walioba.
No comments
Post a Comment