NAPE NNAUYE AMCHANACHANA JAJI WARIOBA NA WENZANKE,ASEMA NI WABINAFSI WANAFAA KUPINGWA
Na Karoli
Vinsent na Sulemani
CHAMA cha
Mapinduzi CCM kimewataka wajumbe wa iliyokuwa Tume ya ukusanyaji wa Maoni ya
Katiba kuachama maramoja Tabia ya kufanya mchakato wa katiba mpya ni mali yao
kwani wao hawana Mamlaka hiyo kisheria.
Kauli hiyo
Imetolewa leo na Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi wa chama
cha Mapinduzi CCM,Nape Moses Nnauye wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari
ofisi ndogo za Chama hicho jijini Dar Es Salaam,ambapo alisema Baadhi ya
wajumbe wa Tume ya Warioba wameufanya mchakato wa katiba kuwa mali yao binafsi.
Kauli hiyo
ya Nape inatokana Mdahalo ulioandaliwa hivi karibuni na Taasisi ya Mwalimu
Nyerere ambao mdahalo huo uliwashirikisha wajumbe mbalimbali wa tume ya warioba
pamoja na mwenyekiti wa tume hiyo ambaye niJaji Warioba mwenyewe,
Ambapo Nape
alisema wajumbe hao katika mdahalo huo walionekana wazi kumbeza Mwenyekiti wa
chama cha Mapinduzi CCM Rais Jakaya Kikwete,kwa kusema yeye ndiye aneuhujumu
mchakato huo wa katiba mpya.
“Mara Kadhaa
na hata katika mdahalo huo,baadhi ya waliokuwa wajumbe wa Tume ya Warioba waekuwa
wakitumia muda mwingi kujaribu kupotosha Umma na kuwashambulia wenye mitazamo
tofauti nay a kwao”
“Kudhihilisha
ukweli huo,sasa wazee hao wameonesha hasira zao kwa kutumia kauli za Dharau na
Kejeli kwa Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa,na wamekuwa wakitumia lusha
kali na hata kutumia uzee”alisema Nape.
Aidha,Nape
alisema kwa sasa chama hicho hakiwezi
kuvumilia hali hiyo,na kitajibu mapigo kila itakapowezekana na kusema pia tabia
ya kumzushia Rais Kikwete alivyokwenda kufungua Bunge Maalum la Katiba kwamba
ndio sababu ya kubezwa ni uongo.
“Nashangaa
sana Mzee wetu warioba navyomsema vibaya Rais Kikwete kwamba alivyokwenda
kuzindua Bunge la katiba ndio kosa, wakati sio kweli Rais naye ni mtanzania
anapashwa kutoa maoni yake kama mtanzania mwengine lakini leo ndio imekuwa
niongwa?”alihoji Nape.
Katika hatua
Nyingine Chama hicho kimewatetea Makada wa chama hicho ambao walionekana kwenda
kinyume na misimamo ya chama hicho,wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa chama cha
Mapinzuzi ccm Bara,Mwigulu Nchemba pamoja na Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe ambao walitaka Bunge hilo la katiba livunjwe kwani limekusa Maridhiono ya
kisiasa kutokana na kutokuwepo upande mmoja wa Kisiasa ambao ni Ukawa.
Badala yake
chama hicho kimesema hayo ni Maoni ya mtu yanapashwa kuheshimiwa na chama hicho
hakina ugomvi na makada wake wowote wanapofikia hatua ya kutoa maoni.
Wakati
huohuo Chama hicho kimesema hakiwezi kutishwa na hatua ya waliyoifanya Umoja wa
kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA kususia na kushindwa kurejea kwenye Bunge
maalum la katiba na kusema hata wasiporejea katiba itapatikana tu kwani hao
ukawa ni watu wachache sana hawawezi kukwamisha mchakato huo.
“Nataka
niwambie watanzania kwamba katiba mpya itapatika hata bila kuwepo hao
wanaojiita Ukawa,kwani ukingalia hiyo hoja wanayosema kwamba 2 ya 3 yawajumbe
itapatikana na ukiangalia wajumbe wabunge hilo wanazidi idadi hiyo kwanini sasa
tuwaogope watu wachache wasiokuwa na hoja ,nawahakikishia katiba Mpya
itapatikana tu”alisema Nape
No comments
Post a Comment