Zinazobamba

MBUNGE MSALITI ANUSURIKA KIPIGO NA WANANCHI,KISA SIASA ZAKE ZA MAJITAKA SOMA HAPA UONE ALIVYONUSULIKA

                                   


 Pichani ni Mbunge msaliti Said Arfi kutoka Jimbo la Mpanda mjini CHADEMA.

Katika hali ambayo inazidi kupigilia msumari wa mwisho kwenye maisha yake ya kisiasa, Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi wa jimboni kwake baada ya kujitangaza kwamba yeye ni CCM huku akiibeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

          Tukio hilo lililotokea Jumatatu ya wiki hii eneo la Maridadi mjini Mpanda limeacha gumzo la aina yake katika viunga vya mji huu huku wananchi wakionekana kuifikisha ukingoni safari ya kisiasa ya mbunge huyo katika namna ambayo almanusura ingemgharimu sana.


           Tukio lilianza kwa Mbunge Arfi kuitisha mkutano wa hadhara aliosema eti si wa kisiasa, ambapo meza kuu aliketi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda anayetokana na CCM 
           viongozi wengine kadhaa wa CCM, ma-VEO na WEOs wa Mpanda, madiwani wawili wa CHADEMA ambao wanajulikana ni wasaliti. Wengine walioandamana naye jukwaani ni viongozi wa CHADEMA waliotimuliwa hivi karibuni kwenye Kamati ya Utendaji ya CHADEMA kwa makosa ya kufanya kazi za CCM kupitia tawi jipya liitwalo ACT.

          Alipopanda jukwaani tu kuanza kuzungumza wananchi wakamtaka kwanza awaambie yeye ni chama gani kwa sababu walikuwa hawamwelewi kutokana na composition ya meza kuu ambayo yeye ndiyo alikuwa ameialika huku akiwaweka kando kabisa viongozi wa chama kilichomdhamini kupata ubunge ambao ameshindwa kuwakuwatumikia wananchi. 

                Baada ya kuombwa aseme yeye ni chama gani, Mzee mzima aka-panic na kuanza kujibizana na wananchi kwenye mkutano wa hadhara eti ule si mkutano wa siasa 

             Makelele yalipozidi akaamua kusema yeye ni gamba yaani CCM. Akawa kama amechokoza nyuki. Yakaanza makelele ya wananchi wakitaka arudishe kadi ya CHADEMA pale pale mkutanoni Mzee akazidiwa kabisa

            Akazidi kusema mbovu kwamba maeneo yote nchini ambako kuna ‘pipooooz power’ (yaani majimbo yanayoongozwa na wabunge wa CHADEMA) hakuna maendeleo ndiyo maana yeye amemua kuachana na hiyo pipooooz power kwa sababu anataka maendeleo jimboni kwake. 

                Akaenda mbali na kuanza kukandia mchakato wa Katiba Mpya kwa kuuponda UKAWA akisema yeye si UKAWA na hautambui umoja huo. Akaiponda Tume ya Warioba akisema haijasema kweli huku akihoji kama kuna mwananchi yeyote anayejua kuwa Tume imesema ukweli anyooshe mkono. Kufika hapo sasa mkutano ndiyo ukavurugika kabisa. 

           Wananchi wakasema hawezi kutuka Tume ya Mabadiliko a Katiba. Hana sifa za kukandia UKAWA, wala hadhi ya kuhoji kazi nzuri ya Jaji Warioba liyozingatia maoni ya wananchi. 

           Akalazimika kufunga mkutano. Wananchi wakamzingira pale pale, wakisema madam ameshasema yeye ni CCM basi awaachie pale pale kadi ya CHADEMA aondoke aende zake. Mzee akawa hawezi kutoka pale. 

             Shukrani kwa Jeshi la Polisi. Zikafika gari tatu za polisi, mojawapo ikiwa imejaa FFU kuja kumuokoa. Polisi walipoona mtiti wa wananchi waliokomaa kwa dhamira moja ‘kubaki’ na kadi ya Arfi, wakalazimika kutumia diplomasia kuwaomba wananchi wamuachie yule mbunge. 

             Akaondoka uwanjani kwa ulinzi wa magari matatu ya polisi yeye akiwa katikati hadi nyumbani ambako pia polisi walilazimika kuweka ulinzi wakijua kuwa kwa hasira mabazo wananzo wananchi dhidi ya mbunge yule kutokana na matukio mengine ya nyuma ya usaliti, wangeweza kumfuata hadi nyumbani.

           Wakati wananchi wakianza kusambaa, mara akapita mdogo wake na Arfi aitwaye Nasoro, ambaye wananchi wenye hasira hawakujua kuwa ni mtu wa misimamo na hayuko na kaka yake katika masuala ya usaliti. Wakamvaa kumaliza hasira zao. 

             Bila watu wengine wanaomjua Nasoro kuwa ni mwanachama na mpenzi mkubwa wa CHADEMA Mpanda kuwahi kumwokoa, tungesema habari yingine muda huu. 

           Wananchi hao wenye hasira waliamua kwenda kumalizia ghadhabu zao kwenye Ofisi za CHADEMA Wilaya ya Mpanda wakikumbushia matukio ya Arfi kushirikiana na MM ‘kuuza’ jimbo kwa Waziri Mkuu na lile la kutupa kadi ya uanachama wakati akiwa bado Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa. 

Kesho yake Jumanne ndipo Arfi akaamua kuukimbia mji na kukimbilia Dodoma.

No comments