HABARI KUBWA LEO--CHAMA CHA ACT WALIA NA RAIS KIKWETE,WATOA TAMKO ZITO SOMA HAPA KUJUA TAMKO GANI HILO
Pichani ni Katibu mkuu wa Chama cha ACT-Tanzania Samsoni Mwigamba picha na Maktaba
Na Karoli
Vinsent
CHAMA cha Kipya cha Kisiasa Nchini Alliance
for Chage and Transparence-Tanzania ACT kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kulivunja
Bunge Maalum la katiba,kwa madai bunge hilo limekosa Uhalali wa Kisiasa.
Kauli hiyo imetolewa mda huu Jijini Dar Es
Salaam,na Katibu Mkuu wa Cha hicho Samson Mwigamba wakati wa mkutano na
waandishi wa Habari,ambapo alisema Chama cha ACT Tanzania kinasikitika kwamba
bunge maalum kuendelea ilihali kundi kubwa la wajumbe wako nje ya Mchakato.
Amesema bila kujali sababu ya kundi
la Ukawa kuwa nje ya Bunge maalumu la Katiba,ACT haiamini kwamba mchakato huu
utazaa katiba bora na yenye kubalika kwa upana bila kujali makundi yote muhimu
kushiriki katika mchakato huo katika ukamilifu wake mwanzo hadi mwisho.
“Ni maoni ya ACT Tanzania tukiendedlea
na mchakato kama ulivyo sasa inawezekana tukapata katiba mpya yenye Uhalali
kisheria lakini itakuwa katiba isiyo na uhalali wa kisiasa wala Jamii na
kwamaana hiyo itakuwa tofauti ya maana na katiba ya sasa na hivyo na kuifanya
nchi kuingia kwenye hasara kubwa ya Fedha za Umma”alisema Mwigamba.
Aidha,chama hicho kimesekitisha
sna na viongozi wa vyama vya siasa wa CCM na vile vinavyounda kundi la UKAWA
kwa kushindwa kwao kupata muhafaka na maridiano kuhusu muunda wa muungano wa
nchi na hata kusababisha kuvurugika kwa mchakato wa katiba .
Vilevile Mwigamba ametaja kuwa ni
Aibu kwamba mchakato Mzima katiba bunge Maalum umetekwa na sera za vyama vya
Kisiasa kuhusu muundo wa serikali ya Muungano badala ya kutafakari na kujadili
Rasimu ya katiba kwa upana na kwa maslai ya nchini na taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyingine chama cha
ACT-Tanzania kimetoa mapendekezo kwa bunge maalum la katiba lisimamishwe ili
kuendelea kutoa fursa ya mazungumzo ya kutafuta muhafaka na maridhiano hadi
baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 pamoja na kufaifanyia marekebisho
katiba iliyopo kwenye vipengele kadhaa.
Ikiwemo kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi
kuwa huru na ya kuonekana,kuruhusu mgombea Binafsi,kushusha umri wa mgombea wa
urais ili kuwapa fursa vijana,kuondoa suala la mafuta na gesi katika mambo ya
muungano ili kuruhusu Zanzibar kuendelea utafutaji mafuta ya gesi kwa uhuru
bila kuingiliwa na Tanzania bara pamoja kuruhusu Zanzibar kuwa na mahusiano na
ushirikiano na kimataifa.
Hali kadhalika,Chama cha
ACT-Tanzania kimewataka wadau wote wakatiba kuungana na kushinikiza mchakato wa
katiba unaoendelea kusimamishwa na kuruhusu mabadiliko hayo machache ya katiba
ya sasa ili kupisha uchaguzi na kuhakikisha taifa linapata muda wa kutosha wa
kuandika katiba bila shinikizo na katika hali ya utulivu
No comments
Post a Comment