Zinazobamba

SAMSONI MWIGAMBA---ADUI YANGU SIO CHADEMA BALI ADUI YANGU NI CCM,AJIBU MAPIGO KUHUSU TUHUMA ZA KUTAKA KUIMALIZA CHADEMA SOMA HAPA KUJUA



 
Katibu mkuu wa chamakipya cha siasa nchini cha Alliance for Chage and Transparence-Tanzania ACT Samsoni Mwigamba picha na Maktba.

  Na Karoli Vinsent
KATIBU mkuu wa chama kipya cha siasa nchini cha Alliance for Chage and Transparence-Tanzania ACT Samsoni Mwigamba ameibuka na kusema adui yake sio chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema bali adui yake mkubwa ni chama cha Mapinduzi CCM,ambacho kimeshindwa kuleta maendeleo zaidi ya miaka 50.
             Kauli hiyo Samsoni mwigamba inakuja siku chache baada ya Madiwani waliohama chadema kwenda chama CCM,harafu baadaye na kurejea tena kwenye chama hicho,na kuibua mipango ilikuwa inapangwa kwa kushirikiana na Makada wa CCM
,           Naibu waziri wa Nisharti na Madini pamoja Viongozi wa Chama kipya cha ACT-Tanzania ya kutaka kumuua Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilbroad Slaa pamoja na Mbunge wa ubungo John Mnyika Chadema.

               Mwigamba alitoa kauli hiyo Jana wakati alipokuwa anaongea na Mwandishi wa Mtandao kwenye Hoteri ya kimatifa ya JB BELMONT Jijini Dar es Salaam,ambapo mwandishi wa mtandao huu alipokuwa anataka kujua mpango ya chama hicho pamoja tuhuma mbalimbali zinatolewa kwenye chama  hicho.
Mwigamba alisema anashangaa sana watu wanaokisema vibaya chama hicho huku waki kihusisha ACT-Tanzania na chama cha Mapinduzi CCM,kwamba wameungana ili waje kuharibu upinzania hapa nchini.
“Kusema kweli hizi siasa za nchini zimekuwa za uzushi sana,sasa mtu anavyosema sisi leo ACT-Tanzania Adui yetu ni Chadema huyo ni muongo mkubwa sana tena anatakiwa kupingwa,kwani wewe (mwandishi) ukienda kufungua duka Arusha harafu ukakuta kunaduka jingine hapo ambalo nalo linauza bidhaa kama zako”
              “ Utasema huyo ni adui yako kweli hapana huyo hawezi kuwa adui yako kwasababu vyama vya upinzani vinaanzishwa kwa ajiri kuundoa utawala ulioko madarakani kwa kushindwa kuondoa umasikini kwa kipindi cha miaka50 na sisi adui yetu ni CCM”alisema Mwigamba.
               Mwigamba kabla kuanzisha chama ACT-Tanzania alikuwa mwanachama wa kada CHADEMA ,ambapo alivuliwa uanachama pamoja na uongozi aliokuwa nao kwenye chama hicho kwa madai yaliodaiwa na uongozi wa Chadema kwamba alikuwa anafanya hujumu kwenye chama hicho.
Kuhusu Chama ACT-Tanzania kuhusika katika mipango ya kuwamaliza viongozi  wa Chadema.
              Mwigamba ambaye ni mwanasiasa anayejiamini alisema taarifa hizo ni za uongo na hajawai kukaa wala kuzungumza  na madiwani hao ambao ni Zakaria Martin Mfuko aliyekuwa Diwani wa Kata ya Masekelo(Chadema) na  Sebastian Peter aliyekuwa diwani kata ya Ingokole(Chadema)
              “Nashangaa sana kuhusu taarifa hizo na hao madiwani naishia kuwaona kwenye magazeti tu  na hata mimi tukikutana nao njiani sizani kama wananijua,hizo ni taarifa niungo mimi nifanye hivyo kwa misingi hipi?alihoji Mwigamba.
                Aidha,Mwigamba aliwataka watanzania kukiamini chama cha ACT-Tanzania kwa madai ndicho chama chenye siasa za kweli  za kuwatoa kwenye umasikini waliokuwa nao.
             Katika hatua nyingine chama hicho Kipya cha Kisiasa Nchini Alliance for Chage and Transparence-Tanzania ACT kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge Maalum la katiba,kwa madai bunge hilo limekosa Uhalali wa Kisiasa.
Chama hicho kimsema bila kujali sababu ya kundi la Ukawa kuwa nje ya Bunge maalumu la Katiba,ACT haiamini kwamba mchakato huu utazaa katiba bora na yenye kubalika kwa upana bila kujali makundi yote muhimu kushiriki katika mchakato huo katika ukamilifu wake mwanzo hadi mwisho.
               “Ni maoni ya ACT Tanzania tukiendedlea na mchakato kama ulivyo sasa inawezekana tukapata katiba mpya yenye Uhalali kisheria lakini itakuwa katiba isiyo na uhalali wa kisiasa wala Jamii na kwamaana hiyo itakuwa tofauti ya maana na katiba ya sasa na hivyo na kuifanya nchi kuingia kwenye hasara kubwa ya Fedha za Umma”alisema Mwigamba.
            Aidha,chama hicho kimesekitisha sna na viongozi wa vyama vya siasa wa CCM na vile vinavyounda kundi la UKAWA kwa kushindwa kwao kupata muhafaka na maridiano kuhusu muunda wa muungano wa nchi na hata kusababisha kuvurugika kwa mchakato wa katiba .
                Vilevile Mwigamba ametaja kuwa ni Aibu kwamba mchakato Mzima katiba bunge Maalum umetekwa na sera za vyama vya Kisiasa kuhusu muundo wa serikali ya Muungano badala ya kutafakari na kujadili Rasimu ya katiba kwa upana na kwa maslai ya nchini na taifa kwa ujumla.


No comments