EXCLUSIVE--SIRI YA UKAWA KUSALITIWA HII HAPA,DK SLAA NAYE ASEMA YAKWAKE KUHUSU USALITI HUO
pichani ni Msaliti wa Ukawa John Shibuda CHADEMA kushoto,akiwa kwenye jukwaa la CCM na Makada wa juu wa chama hicho.picha na Maktaba.
Na Karoli
Vinsent
SIRI ya
kusalitiwa kwa Wajumbe wanaunda Umoja wa kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA
yafichuka mtandao umegundua,Siri hiyo inakuja siku moja kupita baada ya Baadhi
ya Wajumbe wakiwemo , John Shibuda
(Maswa Magharibi), Said Arfi (Mpanda Mjini) na Leticia Nyerere (Viti Maalum)
kuridhia kushiriki vikao vya Bunge Maalum.
Wajumbe hao
wote wanatoka kwenye Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, ambao
wamekwenda kinyume umoja huo wa UKAWA,ambao ni muunganiko wa vyama Vikuu vya
upinzani nchini ambavyo ni Chadema,NCCR,CUF,ND
Pamoja na
Baadhi ya wajumbe 201 waliochaguliwa na Rais Kikwete,ambao wote kwa pamoja
walifikia maadhimio ya kutorejea kwenye Bunge hilo kwa kile wanachokisema
mchakato huo umetekwa na Chama cha Mapinduzi CCM.
Taarifa za
kuaminika ambazo mtandao huu umezipata zinasema Urafi,Tamaa ya Madaraka pamoja
na kutokomaa kisiasa ni mingoni mwa sababu iliowafanya wajumbe hao kuwasaliti
wenzao ambao wenye Marengo ya kuwatetea wananchi wa Tanzania.
Taarifa hiyo
inasema kwa upande wa Mjumbe Leticia Nyerere ni Tamaa ya madaraka imemfanya
awapige chini na kupuuza uongozi wa chama chake cha Chadema na kurejea kwenye
bunge hilo.
Akithibitisha
hayo Rafiki wa Karibu wa mwanamama huyo Leticia nyerere,ambaye aliomba mtandao
huu usilitaje Jina lake, alisema mama huyo amepewa ahadi nyingi sana na Chama
cha Mapinduzi CCM,ikiwemo ukuu wa Mkoa.
“Mimi mwenyewe
nilijua tu lazima Rafiki yangu atarejea kwenye Bunge hilo,maana anataka sana
uongozi huyo,nasikia amehaidiwa vitu vingi sana ikiwemo hata Ukuu wa Mkoa na
CCM wewe unafikili mchezo nakwambia huyo lazima afanye hivyo”
“Anajua
Chadema lazima wamfukuze tu,kutokana na ugegeu aliokuwa nao,na yeye anakwenda
zake CCM,anafikili atapewa utawala huo”kilisema chanzo hicho ambacho ni karibu
sana na Leticia Nyerere.
Kwa upande
Mjumbe mwengine ambaye amewasiliti umoja huo, John Shibuda ni Mbunge wa Maswa Magharibi CHADEMA,naye
alionekana jana kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma na kusaini sehemu ya
mauzulioa na teyali kulipwa na posho.
Akithitisha uwepo wa Mjumbe John Shibuda,
katibu wa Bunge Maalum la Katiba Yahaya Hamis Hamad alisema Shibuda alitoa
taarifa kuwa hatoweza kushiriki kwenye vikao vya kamati kwa madai ana
matatizo ya kiafya.“Shibuda alikuja ofisini kwangu huku mguu wake ukionekana kuwa umevimba hivyo akaomba ruhusa kwenda kupatiwa matibabu, lakini hao wengine wamejiandikisha tu na kuondoka hata hivyo hawajaonekana tena,”alisema.
Duru za Kisiasa zinasema John Shibuda alitabiliwa tu kati ya watu wangewasaliti Ukawa shibuda ni mtu wa kwanza kutokana na kutokomaa kisiasa.
Shibuda ,ambaye aliwai kutajwa kipindi cha nyuma na Makada wa chadema waliofungiliwa Kesi ya Ugaidi na Serikali,kwamba ni miongoni mwa watu waliokuwa wanafanikisha kesi hiyo ya kupambikiziwa ya Ugaidi kwa makada hao,ambapo Shibuda alitajwa kushirikiana na Meya wa Ilemela, Hery Matata kutengeneza Hujuma hiyo.
Lakini shibuda alibuka na kukanusha kwamba taarifa hizo na kusema sio za kweli,lakini licha ya kukanisha taarifa hizo Mwanasiasa huyo anehamahama vyama kila kukicha alionekana mara kwa mra kwenye majukwaa ya chama cha Mapinduzi CCM,akisema vibaya chama chake cha Chadema,na kupelekea kufukuzwa kwenye vikao vya ndani vya chama hicho kutokana na usaliti wake,
Duru hizo ziliziidi kusema kwa siasa za hovyo alizokuwanao John Shibuda ni Ishara tosha kwamba Tanzania inawakati mgumu sana kujijenga Upinzania,na kitendo alichokionyesha jana ni wakati chama Chake kichukue maamuzi magumu ikiwemo kumfukuza hata uanachama.
Mwandishi wa Mtandao huu,alimpotafuta katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa kuhusu ugeugeu huu unaofanywa na wajumbe wanaotoka chama hicho kuwasaliti na kurejea kwenye Bunge hilo ambapo alisema kuhusu Said Arfi (Mpanda Mjini) huyo awezi kumzungumia na kumtaka mwandishi wa Mtandao huu kuwasiliana na Uongozi wa Chadema Mpanda atapata Taarifa kamili.
Na,alipoulizwa kuhusu mjumbe mwengine John Shibuda,Katibu huyo alizidi kusema Shibuda anajulikana kwa tabia yake ya usaliti na chama hicho kinapanga kumchukulia hatua kali ikithibitika kwamba amefanya usaliti huo.
“Kuhusu Leticia Nyerere siwezi kulizungumzia mwandishi, na bado hatujathibitisha na tumesoma kwenye magazeti inasemekana amesaini tu,na tulivyomtafuta kwenye simu sisi kama chadema akasema hayupo Dodoma ila amesaini kwahiyo siwezi kulisema hilo,kuhusu Shibuda huyo anajulikana kwa siasa zake za hovyo tu na chama akiwezi kumvumilia mtu kama huyo na tutamchukulia hatua kali sahivi”alisema Slaa
No comments
Post a Comment