UKAWA KUSALITIWA NA HAWA WENGINE---CCM YAJIPANGA KUWARUBUNI,SOMA HAPA KUWAJUA
Pichani Viongozi wa Umoja wa Kutetea katiba ya Wananchi UKAWA
Na Karoli Vinsent
ORODHA ya majina ya wabunge 16
wanaotafutwa ili Bunge Maalumu la Katiba (BMK) liweze kutimiza akidi ya wapiga
kura watakaoweza kupitisha Katiba imepatikana Umtandao huu umedokezwa.
Wabunge hao ni sehemu ya wabunge 67
kutoka Zanzibar walio miongoni mwa wabunge 201 walioteuliwa na Rais Jakaya
Kikwete kujiunga na BMK wakitoka katika taasisi mbalimbali.
Mtandao huu umeelezwa na vyanzo vyake kutoka ndani ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na BMK kwamba wabunge hao 16 ndiyo watakaofuatwa na kama
watahudhuria na kupiga kura katika vikao halali, Rasimu ya Katiba
iliyotayarishwa na Tume ya Jaji Warioba itaweza kupitishwa na hatimaye
kupelekwa kwa wananchi ili ipigiwe kura.
“Kazi tumemaliza sasa. UKAWA waje au
wasije BMK litakaa na kumaliza kazi yake iliyotumwa na Watanzania. Majina ya
wabunge ambao tunaweza kuwapata yapo tayari, Mtandao umeambiwa na moja
ya vyanzo vyake vya kuaminika juzi Jumatatu.
Majina ambayo Mtandao anayo ni la Yasmine Aluu, Yusuf Omar Chunda, Asha
Makungu Othman, Siti Abasi Ali, Thuwein Issa Thuwein, Sheikh Nassor Mohamed
Ibrahim, Louis Majaliwa na Abdallah Abbas Omar.
Majina mengine ya wajumbe hao kutoka
Zanzibar walio katika BMK wanaotarajiwa kushawishiwa kuendelea na Bunge ni
Biubwa Yahya Othman, Fatma Mohamed Hassan, Sheikh Thabit Jongo, Adilla Hilal
Vuai, Tatu Mabruk Haji, Waziri Rajab, Vuai Ali Vuai na Fat-Hiya Zaharani Salum.
Wajumbe hao, Mtandao huu umeelezwa,
watafuatwa kutokana na vigezo walivyonavyo ambavyo baadhi vimetajwa kuwa ni
kuwa wana CCM, watu kutoka katika familia zilizoshiriki katika Mapinduzi ya
mwaka 1964 na wengine ni wale wanaelezwa kwa “kuwa wasikivu.”
Kazi ya kuzungumza na wabunge hao
inasimamiwa na mmoja wa wabunge mashuhuri kutoka visiwani Zanzibar ambaye
anaruhusiwa kutumia pia watu wengine kuongeza ushawishi.
Ili kupitisha Katiba mpya, BMK
linatakiwa kupiga kura kwa zaidi ya theluthi mbili ya wabunge wake wa Bara na
Zanzibar; lakini wakati CCM ina uhakika wa kupata theluthi mbili Bara,
inahitaji wabunge hao 16 ili kupata theluthi mbili ya wabunge wa Zanzibar.
Baadhi ya wabunge wa BMK kama vile
Profesa Abdallah Safari, wanapinga suala hilo la kutafuta idadi hiyo ya wabunge
pasipo kwanza kuwapo kwa maelewano baina ya UKAWA na CCM.
Hata hivyo, Mtandao huu umeelezwa
kwamba kuna uwezekano wa kupata wabunge zaidi ya hao 16 kutoka Zanzibar, mara
baada ya kufanyika kwa kikao cha Mkutano wa Maridhiano uliopangwa kufanyika
mwishoni mwa wiki hii mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Kikwete pamoja na marais
wastaafu wa Tanzania.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba
Tanzania (Jukata), Deus Kibamba, ameeleza hofu yake kwamba endapo Bunge
litalazimishwa kuendelea, huenda wabunge wa UKAWA wakaenda bungeni kwa minajili
ya kupata posho pekee na si kwa ajili ya kupata Katiba.
“Kabla halijaahirishwa, BMK
lilitumia shilingi bilioni saba. Maana yake linaweza kutumia tena kiasi kama
hicho kwa kulipa watu ambao hawatakuwa na nia ya kutafuta Katiba bali kupata
posho na kututia hasara pasipo sababu”, alisema Kibamba katika mazungumzo yake
na chanzo changu
No comments
Post a Comment