Zinazobamba

WANANCHI WANAHAMU KUBWA YA KUONA BUNGE LA KATIBA LENYE NIDHAMU TENA LIKIWA LIMEENEA: UTAFITI


MKUU WA SHULE KUU YA SHERIA NCHINI KENYA PROF. PATRIC LUMUMBA AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI JUU YA TAFITI ZILIZOFANYWA NA WANAJOPO LILOUNDWA NA JUKWAA LA KATIBA KUBAINI HASA SABABU YA MKWAMO WA KUPATIKANA KATIBA MPYA, AKISOMA MATOKEO YA UTAFITI HUO LUMUMBAAMESEMA WANANCHI WA TANZANIA SASA WANAHAMU KUBWA YA KUONA WAJUMBE WOTE WANARUDI BUNGENI KUTUNGA KATIBA MPYA YENYE TIJA KWA TAIFA LAO NA BILA KUJALI VYMA AMA TAASISI WANAYOIWAKILISHA
MWENYEKITI WA JUKWAA LA KATIBA AKITOA UFAFANUZI MDOGO JUU YA MATOKEO YA UTAFITI WA CHANZO CHA MKWAMO WA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA. UTAFITI HUO UMEFANYWA NA JOPO LA WATAALAM LIKIONGOZWA NA PROF. PATRIC LUMUMBA WA SHULE YA SHERIA KENYA.
SEHEMU YA WAANDISHI WA HABARI WALIOHUDHULIA KATIKA USOMAJI WA LIPOTI YA TAFITI KUHUSU MKWAMO WA BAJETI.



 Utafiti uliofanywa na jopo la wataalam liliundwa jukwaa la katiba kutafiti kiini hasa cha chanzo cha mkwamo wa kupatikana katiba mpya hapa nchini,umemalizika na kubaini makubwa huku sababu kubwa ikiwa ni rais wa Jamuhuri ya muungano akitajwa kuwa ndio Chanzo kikuu.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Daresalaam, kiongozi wa jopo hilo ambaye pia ni mkuu wa shule ya sheria ya Kenya, Prof.Patric Lumumba ametaja sababu hiyo ndiyo iliyoshamili katika vyanzo vyao vyote walivyozungumza navyo

Kadhalika Lumumba amekiri kuwa wananchi wangependa sasa sakata la wabunge ambao walitoka nje kwa sababu ya sintofaham miongoni mwa wabunge wangerudi bungeni ili michango yao iweze kuingizwa katika katiba inayoenda kutengenezwa


No comments