WALIMU WAISHTUKIA RAFU YA SERIKALI YA CCM,SASA WATOA SHARTI GUMU KAMA LISIPOSIKILIZWA KUINGIA KWENYE MGOMO SOMA HAPA UJUE NINI HICHO
Pichani ni Rais wa chama cha walimu Gration Mukoba akifafanua jambo na wandishi wa Habari picha na Maktaba.
Na Karoli
Vinsent
CHAMA cha
Walimu nchini (CWT) kimesema kitapinga kwa nguvu zake au ikiwezekana kuitisha mgomo wa
walimu nchi nzima,endapo kama serikali itapisha sheria ya mpya ya Kupunguza
mafao ya wastaafu wanachama wa Mifuko ya pesheni ya watumishi (PSPF) na
watumishi wanachama wa LAPF.
Tishio hilo limetolewa Leo Jijini Dar
es Salaam,na Rais wa Chama cha Walimu (CWT) Gratian Mukoba wakati wa Mkutano na
Waandishi wa Habari,ambapo alisema chama hicho baada ya kupata pendekezo kutoka
Wizara ya Kazi na Ajira kwa kushirikiana na Mamlaka ya mifuko ya Jamii (SSA)
kuhusu punguzo hilo kwa watumishi wa umma ikiwemo walimu.
Ambapo chama cha walimu katika kikao
chake cha kamati ya utendaji ya Taifa(KUT) kilichokaa mjini Morogoro walijadili pendekezo
hilo na kuja maamuzi ya kupinga kwa nguvu zote mpango huo ambao unalenga
kuwadhulumu walimu pamoja wafanyakazi wengine mafao ya kustaafu kama
utapitishwa kutungiwa sheria.
Mukoba,alizidi kusema mpango huo
ukipitishwa na kuwa sheria utapunguza kinua mgongo cha walimu na watumishi
wengine wa umma.
“Hatuwezi
kukubali mpango huu,kwani utazidi kumfanya mwalimu awe masikini zaidi,mpango
huu utamaliza kiiunua mgongo cha walimu,kwani zaidi ya nusu kile wanachokipata
kwa sheria iliyopo sasa,wakati wanajua watumishi hawa wanaishi katika hali ya
umasikini wa kutisha”alisema Mukoba.
Mukoba
ambaye kitaaruma ni Mwalimu,aliyataja maeneo hayo ambayo watayapinga kwa nguvu
zote ikiwemo
Kupunguza malipo ya Pesheni ya mkupuo yanayolipwa na
mifuko ya PSPF na LAPF kutoka asilimia 50 ya sasa hadi asilimia 33.3 ya mshahara
wa mwezi wa Mtumishi kabla ya kustaafu,
Vilevile alizidi ya kuyataja maeneo
mengine ni kupunguza makadirio ya Umri
wa kuishi kwa mwanachama baada ya kustaafu toka miaka 15.5 baada ya kustaafu
hadi miaka 12.5,
Katika hatua nyingine chama hicho cha
walimu kimesema wamegundua sababu ya Serikali kufanya Rafu hiyo mbaya kwa
Watumishi wa umma ni kutokana na Serikali kudaiwa pesa nyingi sana.
“Tumechunguza tumegundua sababu ya
Serikali kuendelea kuwakandamiza watumishi hawa wa Umma ni kutokana na serikali
zaidi ya Trilioni 7,”
“Kwa pamoja tunaiomba sana serikali
isitishe mpango huu wanaotaka kuleta,na kama wanatafuta njia nyingine kuiokoa
mifuko hii,basi watafute njia nyingene”alisema Mukoba
No comments
Post a Comment