URAIS NDANI CCM NI KAA LA MOTO,NAYE WAZIRI MKUU PINDA NAYE AJITOSA RASMI AANZA KUPANGA MAKUNDI YAKE SOMA HAPA UONE JINSI ALIVYOKAMIA
Picha ya Waziri Mkuu Mizengo pinda,picha na Maktaba
Na Karoli
Vinsent
UWEZEKANO wa chama cha Mapinduzi kugawanyika
kunakosababishwa na wasaka Urais ndani ya
chama hicho,uwezekano huo unazidi kuonekana baada ya hivi sasa naye Waziri mkuu, Mizengo Pinda naye kujitosa
Rasmi kwenye Dibwi hilo na kujihakikisha anashika nafasi ya Kumrithi Rais
Jakaya kikwete,anayemaliza mda wake mwakani 2015,Mtandao huu umedokezwa.
Waziri mkuu Mizengo Pinda,anaungana na
Wasaka urais ndani ya chama hicho ambao nao wanasaka urais kufa na kupona ni
Waziri mkuu aliyejiuzuru,Edward Lowassa,Waziri wa ushirikiano na Uhusiano wa
Afrika Mashariki,Samwel sitta,Naibu waziri mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,January
Makamba,Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu,Fredrick sumaye,pamoja Waziri wa
mambo ya Nje,Berdard Membe.
Taarifa ambazo Mwandishi wa Mtandao
huu,amedokezwa Zinasema kwa Waziri Mkuu Pinda,ameanza kuanda vikao vya siri na
Kuhakisha anashika nafasi ya kumrithi Rais Kikwete,ambapo Pinda anajivunia ukaribu
aliokuwa nao Rais kikwete huku akijiona unaweza kumpa mwanya na sifa ya kuweza, kuchukua Nafasi hiyo ya Urais.
Taarifa hizo za ndani zinasema Waziri
mkuu huyo teyali ameshafanya Vikao vya Siri,ambapo amefanya vikao,Jijini Dar es
Salaam,pamoja na Dodoma,kabla ya kwenda Jijin London,nchini Uingereza,wiki
zilizopita.
Chanzo hicho kilizidi kusema katika
kikao kimoja kilichofanyika Jijini Dar Es Salaam,kilihudhuriwa na Wanasiasa Mbalimbali
,huko akiwemo meya mmoja kutoka jiji la Dar Es Salaam ambaye jina lake
tunalihifadhi,
Katika Kikao hicho Pinda alitumia
nafasi kubwa ya kuwambia wanasiasa walikuwemo kwenye kikao hicho,kwamba a
lazima ndoto yake itimie kushika nafasi hiyo kubwa ya nchi,huku Waziri mkuu
huyo alitumia mda mwingi akielekeza maneno kwa Wasaka Urais ndani ya chama
chake kwamba hawana sifa.
Kuibuka huko kwa Mizengo Pinda kumekuja
huku ikiwa bado Kamati kuu ya chama chama Mapinduzi CCM,kikiwa kime kimewazuia
wanachama wake kutotangaza nia yoyote kwenye Nafasi Urais,
Katibu wa Itikadi wa Chama cha Mapinduzi
CCM Nape Nnauya,alizidi kupigia msumari suala hilo,Alhamisi iliyopita Wakati wa
Mkutano wa Waandishi wa Habari,ambapo alisema chama chake kinafuatalia kwa
ukaribu mienendo ya Wanachama waliopewa Adhabu na Kamati kuu ya (CC)na kuongeza
kwamba Kamati kuu itapitia upya wanachama wake sita waliopewa karipioa kwa kosa
la kutangaza Nafasi mapema.
Kuibuka huku kwa Waziri mkuu mizengo
Pinda kunazidisha Homa kwa Wasaka Urais Ndani ya Chama hicho Kikongwe Barani
Afrika,huku kukiwa na Sintofanu kuhusu nafasi hiyo.
Ambapo Taarifa ambazo mwandishi
mtandao huu amedokezwa zinasema Waziri wa uhusiano wa Afrika Mashariki,Samwel
Sitta,jumamosi iliyopita alifanya Kampeni ya chinichini kampeni alifanya huko
mkoani Kagera ambapo alipokuwa Mgeni wa Rasmi katika mahafari ya Chuo cha
Wauguzi cha Mugana,kinachomilikiwa na kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba.
Katika Mahafari hayo,Sitta alitumia mda
mwingi kumtupia vijembe msaka Urais Mwenzake ambaye ni Waziri mkuu aliyejiuzuru
Edward Lowassa kwa kusema hana sifa ya kuwa kiongozi katika nchi hii kutokana
na vitendo vyake vya ufisadi vya nyuma.
“Kama watajitokeza watu waongo wenye
rekodi Mbaya na wasiokuwa Waadilifu,itabidi na sisi wazee tujitose katika
kinyang’anyiro hicho kwani hawa wezi hawafai kushika nafasi yeyote katika nchi
hii”
“Watu hawa hukiwatazama kabisa
wanaonekana ni wezi na walaghai wengine wanarekodi mbaya katika utumishi
wao,yuko mwengine alihujumu mpaka nchi,eti leo anasimama kwenye majukwaa anataka
urais”alisema Sitta.
Naye Msomi wa masuala ya Kisiasa nchini
kutoka chuo Kikuu cha Dodoma,Seiph Yahaya.alisema kitendo cha Waziri mkuu
mizengo pinda kujitosa katika nafasi hiyo ya kuwania urais,ni ishara tosha
chama cha Mapinduzi CCM,kinaweza kugawanyika.
“Sikiliza mwandishi,tunajua kabisa
Rais Jakaya Kikwete anamuandaa Mizengo pinda,ashike nafasi hiyo ya Urais,na mimi
nakwambia kama Rais leo tupangiwe na
Rais Jakaya Kikwete,basi chama hiki akifiki mbali lazima kigawanyike tu
utashuhudia tu mwakani”alisema Yahaya
No comments
Post a Comment