Zinazobamba

MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI KWA TIKETI YA FRELIMO AJA KUCHOTA MAUJANJA CCM, ADAI CHAMA CHAKE KINAHISTORIA NDEFU NA NCHI YA TANZANIA

Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari ambao walitaka kufahamu mahusiano yao na CCM pamoja na namna Demokrasia inavyoendeshwa nchini Msumbiji,Mheshimiwa Nyusi alisema mahusiano yao na CCM ni mazuri na ya kihistoria Tangia wakati wa mapambano ya Ukombozi,alipoulizwa kuhusu uwezo wake wa kuongea Kiswahili vizuri alisema wakati wa mapambano ya Ukombozi aliwahi ishi Tunduru na Nachingwea nchini Tanzania.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mgombea wa Urais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi kwenye hotel ya Golden Tulip ambapo alikuwa na mazungumzo naye .
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria akisalimiana na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi, kabla ya kuanza mazungumzo kwenye hoteli ya Golden Tulip.

 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dr.Asha-Rose Migiro(Kulia),Katibu wa NEC Oganizesheni Dr.Mohamed Seif Khatibu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Maofisa wengine wa Chama Cha Mapinduzi kwenye meza ya mazungumzo na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi na Ujumbe wake kwenye ukumbi wa  Nyerere,Golden Tulip Hotel.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dr.Asha-Rose Migiro(Kulia),Katibu wa NEC Oganizesheni Dr.Mohamed Seif Khatibu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye meza ya mazungumzo na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi na Ujumbe wake kwenye ukumbi wa  Nyerere,Golden Tulip Hotel.
MAPOKEZI YAKE JANA YALIKUWA HIVI
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimlaki Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi cha FRELIMO, Filipe Nyusi alipowasili leo jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya ziara ya siku tatu, kusaka kura kwa wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania kufuatia kampeni za Urais zinazoendelea nchini kwake.
Mgombea huyo wa Urais Filipe Nyusi akimsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia alifika Uwanja wa Ndege pamoja na Kinana. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
 Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Filipe Nyusi akisalimiana na wana-CCM waliofika kumlaki Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Kulia ni Mwenyeji wake, Abdulrahman Kinana
 Nyusi akidhihirisha furaha kwa mapokezi aliyopata
 Mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji akiwa na Mwenyeji wake, Kinana wakati wa mapokezi yaliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
Filipe Nyusi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mapokezi, Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
 Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mama Maria Nyerere (watatulkushoto) akiwa na ugeni wa mgombea huyo wa Urais nchini Msumbiji, Filipe Nyus (wapili kushoto), nyumbani Mwalimu, Msasani, Dar es Salaam. Kushoto ni Kinana
 Mama Maria Nyerere akimsalimia Mtoto wa Rais wa Kwanza wa Msumbiji Samora Machel, Samora Samora ambaye alifuatana na mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji.
 Mama Maria Nyerere akizungumza na mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji Filipe Nyus (wapili kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana
 Nyusi na Kinana wakimsikiliza kwa makini Mama Maria Nyerere wakati wa mazungumzo hayo
Samora Samora akizungumza na Binti wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, wakati wa ugeni huo nyumbani kwa  Mama Maria Nyerere, Msasani Dar es Salaam

Hakuna maoni