Zinazobamba

HABARI ILIYOTIKISA JIJI,KAMPUNI YA VITA FOAM YATUZWA CHETI CHA KIMATAIFA KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATANZANIA, YAWA KAMPUNI YA KWANZA KUTUMIA BAR CODE YA KITANZANIA NA KUFANIKIWA


IMG_0142
Mkurugenzi wa kampuni ya VITAFOAM akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habarimapema hii leo,Kulia kwake ni meneja biashara anahusika na utoaji wa cheti cha Ubora wa kimataifa Bw. Boniface Kanemba
Kampuni ya utengenezaji magodoro ya Vita Foam imepokea cheti cha kimataifa cha uthibitisho yaaani  ISO 9001:2008 na bar code ya Tanzania kutokana na kutimiza viwango vya usimamizi wa ubora kinachotambulika kimataifa.
 Makabidhiano hayo yamefanyika hii leo hapa jijini Daresalam kati ya maneja masoko anayehusika na utoaji wa cheti cha Ubora hapa nchini Bw. Boniface Kanemba na mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya kutengeneza magodoro ya Vitafoam, Bw. Suraj Chandalia
Akikabidhi cheti hicho kwa mkurugenzi waMagodoro ya Vitafoarm, Meneja wa IMSM (ISO management system), amesema hatua ya kuwakabidhi cheti cha ubora kwa kampuni ya vita foam leo imefikiwa baada ya kuona ubora wao wa magodoro wanayoyauza kwa watanzania na kukili wazi kuwa huduma inayotolewa na kampuni hiyo ni ya kimataifa kwa sasa,

Aidha Kanemba amewashuri wafanyakazi na watendaji wa kampuni hiyo kuacha kubweteka kwani kupata cheti hicho ni hatua moja na kukimaintain ni hatua nyingine hizo lazima wakaze buti waweze kutoa huduma bora tena iliyo endelevu kwa watanzania ili waendelee kupata cheti hicho cha ubora kwa miaka mingine ijayo,
Akizungumzia hatua ya kampuni yake kuchaguliwa kuwa kampuni ya kwanza kutoa huduma bora ya magodoro kwa watanzania na kupatiwa cheti hicho, Mkurugenzi wa kampuni hiyo amesema kwanza amefurahishwa na hatua hiyo na kukiri hadharani kuwa watahakikisha wanatoa huduma iliyobora muda wote kwa watanzania ili waendelee kuwa bora wakati wote
"Sisi kwanza tunashukuru kwa jitihada zetu kuonekanakimataifana kutufanya tuwe kampuni ya kwanza na ya kipekee ya kutengeneza magodoro Tanzania kufikia uthibitisho ISO 9001:2008."Alisema Bw.Chandalia
“Cheti hicho kimefanyiwa utathimini na kupitishwa na bodi maalum ya uthibitisho linalojulikana kimataifa, QAS international na ndicho cheti kinachopanga vigezo kwa ajili ya mfumo wa usimamizi bora na kinatoa mfumo muhimu ya kuboresha ufanisi wa kampuni, kupunguza hali ya hatari na kuongeza nafasi,” alisema Chandalia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko Tanzania kutoka kampuni ya GS1na Mkurugenzi wa Bar code hapa nchini Bw,Mabamba Malegesi wakizungumzia hatua ya kuwakabidhi bar code maalum kampuni ya Vitafoam ya kutambulisha bidhaa hizo kama zimetengeneza hapa nchini, amekili kuwepo changamoto kwa makampuni makubwa kutokuonyesha moyo wa kutumia bar code za Tanzania ili bidhaa hizo ziweze kujulikana kama zimetoka katika taifa hili la Tanznai
 Bamba malegesi amesema katika suala zima la muitikio wa makampuni kutumia bara codeza kitanzania bado uko chini na kwamba hayo yanasabishwa na makampuni makubwa kukaa kimya katika kuchangamkia bar code za Kitanzania,
Mpaka sasa, Malegesi amesema ni makampuni 750 tu ambayo yamefanikiwa kuchukua bar code ya Kitanzania huku makampuni zaidi ya 100,000 bado yakiwa yanasuasua kuchhukua bar code ya Kitanzania,
Fullhabari ilipotaka kujua ni kwa nini makampuni makubwa hapa nchini hayako tayari kuchukua bar code za kitanzania na badara yake inatumia bar code za nchi za nje, Malegesi amekiri makampuni hayo kutumia barcode za nchi za nje na hiyo inatokana na wao kutokuwa tayari kutumia bar code za Tanzania kwasababu wanazozifahamu wenyewe,
Aidha akizungumzia kuhusu sheria inasema nini kama kampuni haitaki kutumia bar code za taifa lake, Malegesi anasema sheria hakuna za kuendesha barcode hivyo nchi inaendeshwa kwa moyo wa kizalendo,
Ametumia fulsa hiyo pia kuwaomba makampuni makubwa kujitokeza kuchukua barcode za Kitanzania ili bidhaa za kitanzania nazo zifahamike nje ya mipaka ya taifa hili,
Mfano majo ya Kilimanjaro, barcode yake ni nchi ya Bergium, sasa kama tunayauza huko nje lazima yatajulikana kuwa yametoka katika taifa hilo, ni lazima watanzania tubadilke aliongeza Bw.Malegesi. 

Hakuna maoni