MSAKA URAIS LOWASSA,AZIDI KUPATA PIGO,SASA WAPAMBE WAKE WAANZA KUJIONDOA,SOMA HAPA UJUE JINSI ALIVYOGEUKWA
Pichani ni Waziri mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa
Na
Karoli Vinsent
KILE kinacho
tafsiliwa kwamba Wapambe wa Msaka Urais Edward Lowassa wameanza kumgeuka na
kuanza kujiondoa katika harati zake za kuchukua usukani wa Juu wa uongozi wa nchi
kwenye uchaguzi mkuu mwakani 2015 ndani ya CCM,zimeanza kuonekana Mtandao huu
umebaini.
Mtandao huu umedokezwa kwamba
aliyekuwa mpambe wa Msaka huyo Urais Edward Lowassa,ni aliyekuwa Katibu Mkuu
mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM,Yusuf Makamba teyali amejitoa kwenye kundi
la kumpigania Waziri mkuu huyo aliyejiuzuru.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika
ambazo mwandishi wa Mtandao,amezipata zinasema awali Mzee Makamba alikuwepo
katika upande ambao ulijitosa kuhakikisha Lowassa anachukua Urais katika
uchaguzi mkuu mwakani 2015,lakini sasa ameamua kujiondoa.
Chanzo hicho makini kinasema sababu ya
Katibu huyo wa Mstaafu wa CCM,kujiondoa ni Kutokana na Mwanae January
Makamba,ambaye teyali ametangaza nia y a kuwania nafasi hiyo Urais na teyali baadhi ya watu wameanza
kumuunga mkono kutokana na uamuzi wake wa kujitosa katika nafasi hiyo.
January makamba ambaye ni Naibu waziri
wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,alitangaza uamuzi huo wiki iliyopita
wakati akifanyia mahojiano na Shirika la Utangazaji la BBC,aliitaja nia yake
kugombania nafasi hiyo ya Amiri Jeshi mkuu,na kusema sasa ni wakati wa Vijana
kushika nafasi hiyo.
Mtoa taarifa huyo aliuombia mtandao
huu kwamba Mzee Makamba teyali amejitoa
katika upande wa Lowassa na teyali ameacha pigo kwenye harakati hizo.
“Sikufichi hizo taarifa ni za kweli
mpambe mwenzetu tuliyekuwa naye wakati tukipigani mzee wetu huyo lowassa
kuingia ikuru,eti naye amejitoa na kuanza kumsapoti mwanae Janury
makamba,ambaye naye ameanza kukubalika kiasi chake kwa watu mbalimbali ikwemo
wachambuzi wa kisiasa”
“Na hili nakuhakishia ni pigo kubwa
sana kwa Mzee wangu Lowassa kwasababu nafasi aliyekuwa anaifanya ni kubwa sana
katika harakati hizo ndugu”alisema mtoa taarifa huyo.
Naye Mjumbe Halmashauri kuu ya chama
cha Mapinduzi CCM NEC,kutoka mikoa ya Kanda za juu kusini aliyezungumza na Mwandishi
wa Mtandao huu kuhusu hali hiyo,kwa sharti la kutoandikwa Jina mtandaoni
alisema lowassa anawakati mkugumu sana katika harakati zake kwani teyali nguvu
yake kwa kundi lake inaanza kumeguka.
“Mzee yusufu Makamba teyali amejiondoa
sasa katika upande wa kundi la lowassa .sasa utagemea nani anaushawishi katika
kundi la lowassa,kwa hili tusitegemee jipya kwenye Nafasi yake,hebu ona jinsi
anavyopigwa vita na kila Kada wa CCM,”alisema Mjumbe huyo.
Kwa upande wake Msomi wa Masula ya
Kisiasa kutoka chuo Kikuu Dodoma,Seiph Yahaya alisema waziri mkuu aliyejiuzuru
Edward Lowassa anawakati mgumu sana kuingia Ikulu kwani kila msaka urais
anayeibuka anampinga yeye ,na kwa mtazamo huu chama cha CCM,uwenda kikapasuka
vibaya wakati wa kumteua mtu anatakayeshika nafasi ya urais kwenye uchaguzi
mkuu mwakani 2015.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni