WATOTO ZAIDI YA 800 WALAWITIWA KWA KIPINDI KIFUPI TU CHA MWAKA JANA, LHRC WATOA TAMKO KALI
Kaimu wa LHRC Wakili Sungusia akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika huko Kijitonyama ofini kwake |
Hali ya kutothaminiwa kwa haki za watoto hapa nchini imeendelea kuwa tatizo baada yawatoto zaidi ya laki nane kuonekana kulawitiwa huku wanaohusika na ushenzi huo wakionekana wanalandalanda bila kuchukuliwa hatua za msingi hoja kubwa ikiwa ni uhusiano wa karibu kati ya mtoto aliyerawitiwa na mlawiti,
Akizungumza na waandishi wa habari hapa Ofisini Kwake katika
maazimisho ya siku ya mtoto wa afrika hapa nchini , Kaimu mkurugenz wa Kituo
Cha sheria na haki za binadam, Wakili Harodia Sungusia amesema haki za mtoto
hapa nchini zimekuwa zikidorola kwa asilimia kubwa ingawaje kuna jitihada za
kulinda haki za watoto,
Sungusia anasema Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa jumla ya
watoto 863 wamelawitiwa lakini takwimu hazisemi ni jumla ya waharifu wangapi
ambao wamefikisha katika mahakama na hukumu ngapi zimeshapitishwa dhidi ya
ushenzi huo unaofanywa na watanzania wachache kwa watoto hao wadogo,
“Tayari tunatakwimu hapa juu ya haki za watoto
zinavyovunjwa, lakini hatujui ni wangapi wamechukuliwa hatua, tunadhani sasa
wizara ya watoto lazima waliangalie hili kwa makini kwani kunyamaza kimya ni
sawa na kuvunja haki za watoto ambao ndio taifa la kesho,” Aliongeza Sungusia
Sungusia amebainisha baadhi ya sababu za haki za watoto
kuminywa kuwa ni pamoja na walezi, ndugu, na wazazi wao wa damu kutokuwa tayari
kuwafichua wanovunja haki za watoto, kwa mfano hawa ambao wanalawitiwa, kama
kuna mtu mwenye ujasiri basi haki ya mtoto ingepatikana
“Unakuta mtoto amelawitiwa na baba mdogo au shangazi yake
ama baba ya ke mkubwa sasa mzee kulifikisha suala hilo mahakamani anaona ni
shida hivyo ananyamaza kimya na maswala hayo yanamaliza kimila na mwishowe haki
ya mtoto inapotea kisa tu aliyefanya unyama huo ni ndugu yake wa damu, kwa
kweli hili alikubaliki,”Aliongeza Wakili Sungusia
Aidha katika hatua nyingine Wakili Sungusia ametaja haki
zingine ambazo mtoto wa afrika amekuwa akionewa ni pamoja na watoto
kutumikishwa na kufanyishwa kazi hatarishi. Utafiti unaonyesha kuwa mpaka sasa
watoto wa Kiafrika bado wanafanyishwa kazi ngumu na hatarishi kama zile za
migodini,viwandani na wengine wamelazimishwa kujiunga katika majashi ya waasi
kama yale ya Joseph Koney wa Uganda, na M23 ya Congo na vikundi vya kiagaidi
vya Alshabaab nchini Somalia
Kumekuna na mwendelezo wa watoto kubaguliwa na
kunyanyapaliwa, hii ni tatitzo kubwa kwa ustawi wa watoto wetu hasa hapa barani
Afriaka, ambapo sasa imekuwa ni kawaida kwa wazzazi na walezi kuwaficha watoto
wao kisa ni walemavu wa viungo fulanifulani hatua inayomfanya mtoto aliyefichwa
kukosa haki yake ya msingi ya Elimu,Afya,Malezi bora, na LIshe
Kutekwa , kuuzwa na kusafirishwa kimagendo , Afrika bado
inachangammoto kubwa ya watoto wake kutekwa na kupelekwa sehemu mbali ili wakauzwe kwa
lengo la kuwatumikisha katika nchi za ng’ambo, hakika hili ni tatizo ambalo
linahitaji utatuzi wa haraka kama kweli tunataka kulinda haki za mtoto Wa
Afrika.
LHRC WATOA WITO KWA VIONGOZI WA DINI, kuanza kulinda haki za
watoto kwani watoto ni taifa la kesho,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni