Zinazobamba

Pathfinder international wazindua huduma mpya, sasa wawasaka wagonjwa wa TB kwa simu

http://www.pathfinder.org/assets/images/wrpr/pf_logofooter.png



Mpango wa kuibua wahisiwa wa ugonjwa wa TB hapa nchini umezinduliwa rasmi  mapema hivi karibuni katika wilaya ya Kinondoni, dhamira kubwa ikiwa ni mpango wa kuwatafuta waathirika wa ugonjwa wa TB katika manispaa ya hiyo ili waweze kufikisha hosptari na kupatiwa huduma

Akizungumza na mtandao huu Deputy country representatives  wa  PATHFNDER intenational  Dr. Pasiens Mapunda amesma kuwa wameamua kuzindua mpango wa kuwasaka waathirika wa ugonjwa wa TB kokote pale walipo ili kuweza kuwasaidia kuimalisha afya zao ,

http://www.pathfinder.org/assets/images/news/mHealth-Tanzania-audience.jpg
Hapa wananchi wakituma ujumbe mfupi .

Wakati akizungumza na mabibi na mabwaa afya wa ngazi ya mtaa katika wilaya ya Kinondoni, Mapunda amesema, ugonjwa wa TB bado ni tishio na kwamba ili kunusuru maisha ya watanzania wenzetu tunaona ni vyema sasa wagonjwa watoe ushirikiano wa kutosha kwa kutoa taarifa kwa nyia ya simu yake ya mkononi


Akizungumzia mikakati ya kuwatafuta wagonjwa hao, Mapunda amesema ili kuwafikia wananchi wengi na wao waweze kutoa taarifa zao kwa wakati wameamua  kuzindua huduma  hiyo kwa njia ya simu ambapo mwananchi anaweza kutuma taarifa zake kuhusiana na hali anayoiona kupitia namba  15077,


Mapunda amesema mteja anashauriwa kutuma ujumbe mfupi kwa kuandika Neno TB kasha atume Kwenda 15077 na kasha atatumiwa maswali anayotakiwa kujibu ili kubaini hali ya mgonjwa anayetuma taarifa hizo

Mapunda anasema, Kupitia mpango huu mpya wanategemea wananchi wengi watajitokeza kwa wingi kutaja matatizo yao kuhusiana na ugonjwa huu ili waweze kutambulika na kusaidia kupata huduma inayostahili kwa wakati na bila malipo,

Aidha kuhusiana na Gharama za kutuma meseji kwa njia ya mtandao kupitia simu yake ya mkononi, Mapunda amesema Mgonjwa hatahusika na gharama yeyote, hivyo anawashauri wagonjwa wasisite kutoa taarifa mapema kupitia njia hiyo mpya waliyoibuni kwa sasa,

Naye afisa mipango wa shirika la PATHFINDER intenational, Bi Anna W.Mwakibete, ameweka bayana mbele ya mwandishi wa habari hizi kuwa shirika la Pathfinder International limedhamilia kuwasaidia wagonjwa wa TB na hivyo anawashauri watanzania hususani wakazi wa wilaya ya Kinondoni na Mitaa yake kutoa taarifa juu ya ugonjwa huu kwa mgonjwa anayeonekana kuwa na dalili za TB ili aweze kupatiwa msaada wa haraka ,

Ukiona kuwa kunamgonjwa nyumbani kwako tunaomba tutumie taarifa kupitia simu yako ya mkononi kwa kuandika ujumbe mfupi ukianza na neon TB kasha tuma kwenda namba 15077 kisha jibu maswali yatakuja na baada ya hapo utafahamisha hospitari ya kwenda,

Mpaka sasa Mapunda amesema huduma hii ya kutafuta wagonjwa wa TB kutumia simu inapatikana katika  kata 13 za wilaya ya Kinondoni, ambazo ni kata ya Goba,Kijitonyama, Makuburi,Makurumla, Mburahati, Tandale,Hananasif,Kinondoni,Makumbusho, Mbezi-Kimara,Mwananyamara,Kawe na mabibo.

“Tumeanza majaribio ya mpango huu hapa Kinondoni na tukiona mafnikio basi tutakwenda Tanzania nzima, sababu sisi lengo letu ni kuona watanzania hawasumbuliwi na ugonjwa huu wa TB” alisema Mapunda




No comments