UZINDUZI WA KUFA MTU KUFANYIKA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI, SOMA HAPA USIPITWE NA WAKATI...

Ni siku ya Ijumaa tarehe 6 june,ndani ya ukumbi mkubwa wa MAKUTI HALL
chuo cha usafirishaji ambapo wanavyuo kutoka sehemu mbalimbali
wakichanganyika na watu wao katika kupata elimu,burudani sambamba na
uzinduzi wa nguo za designer Mchox ziitwazo DUFU,akiongea na Swahili24
Blog,Masoud Mohammed ambaye ni mratibu wa onesho hilo amesema maandalizi
kwa kiasi kikubwa yamekamilika na anawashukuru wadhamini wote walioweza
kuongeza nguvu kwenye show hiyo akiwataja kama ifuatavyo Serengeti
Breweries,Global Publishers,Swahili24 blog,Lin Collection,Epiq Media
Production,Mchox Boutique,Omega Incorporation,Tayoa,Cocacola Kwanza
ltd,Mwananchi Communication,National Institute of Transport,Pilipili
Entartainment ltd na Burn Records.
Zoezi la utoaji damu litaenda sambamba na unywaji wa soda,bia na
vinjwaji vingine vya kuirudisha damu iliyotolewa.Pia Masoud aliongeza
kwamba kwenye bonanza hiyo kutachezwa mechi ya kugombania ngao ya hisani
ambapo mshindi atapata kikombe na pesa taslimu.
Show hiyo itahamia usiku ambapo mbunifu wa mavazi Fadhil Mchongoma a.k.a
Mchox atazindua mavazi yake akisindikizwa na wanamuziki na watu maarufu
kibao ambao kwa uchache ni Vedasto,Country Boy,Babuu,Shadoo,Man Afro
huku kwa mara ya kwanza Ayoub Alex a.k.a Sabodo anasimama mbele ya watu
zaidi ya 400 akichekesha.
Upande wa watu maarufu watakao show luv kwa Red Carpet ni Monalisa,Natasha,Sheddy Clever,Tinny WHITE,JB,na wengine kibao.
Mwisho mratibu alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wadhamini wakuu wa
tamasha hilo ambao ni Serengeti Breweries,Lin Collection,Swahili24
blog,Omega incorporation,mkuu wa chuo cha usafirishaji,mkurugenzi mkuu
wa Pilipili Ent.,Mchox Boutique,Epiq media Production,cocacola kwanza
ltd,na tayoa.

..






No comments
Post a Comment