AZAM TV WAVUKA KIZINGITI CHA KWANZA
Katika kile kinachoonekana ni muitikio mkubwa wa wananchi wa kitanzania juu ya huduma zinazotolewa na Kituo kipya za Azam Tv, Inaelezwa kuwa mpaka sasa kituo hicho kimefanikiwa kuweza kuuza vigamuzi vyake zaidi ya lakini moja hapa nchini mpaka hiyo jana jioni
Akizungumza na Mtandao huu, mtendaji mkuuu wa Azam media amesmma kuwa kituo chake kimefanikiwa kuweza kuvuka malengo waliyojiwekea kwa haraka sana na isivyo kawaida katika biashara ya TV, na kusema hatua hiyo inaonyesha ni namna gani watanzania wameikubali huduma itolewao na kituo hiko kipya hapa nchini,
Kwa kipindi cha miezi sita, tayari Azam media imefanikiwa kuuza ving'amuzi vyake zaidi ya laki moja, kitu ambacho amesema si mafanikio madogo ukilinganisha soko lenyewe lilivyo kwa sasa, kwani kwenye soko tayari kunawatu wanatoa huduma kama hii
Kwa kweli kwanza tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono katika biashara hii, sisi nguvu yetu kubwa ni watanzania kwani wao ndio watumiaji wa huduma zetu, na tunashawishika kusema kuwa tutaendelea kuwapa huduma iliyo bora tena ya kiwango cha juu .
Tunafahamu kuwa watanzania wametuamini na ndiyo maana wanakuja nakuchukua ving'amuzi vyetu, tunachoweza kusema kwa sasa kuwa tumedhamilia kuwapa huduma iliyo bora sana na kuna mambo makubwa yanakuja hivyo kaaaeni mkao wa kula,
Tanzania kwa sasa soka lake litaonekana na mataifa mengine kupitia Azam Tv hii ni kutokana na ukweli kuwa Tayari kituo cha Azam media kimeshaanza mikakati ya kupata wateja nje ya Tanzania,
Wakati huohuo habari mpya ni kwamba KAMPUNI ya Azam Media imetangaza kuwa tayari imeshatuma fedha kwa Bodiya Ligi kwa ajili ya msimu wa ligi wa Vodacom kwa mwaka 2014/ 2015. Fedha hizo zimetolewa mapema zaidi kwa ajili ya kusaidia maandalizi mapema kwa timu kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba wa miaka mitatu ya udhamini wao katika ligi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za Azam zilizopoTazara, Dar es salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, RhysTorrington, alisema kuwa kampuni hiyo inavutiwa na aina nzuri ya
ushirikiano kati yake na bodi ya Ligi.
ushirikiano kati yake na bodi ya Ligi.
Alisema kuwa kupitia bodi hiyo Azam imepiga hatua kubwa katikakufanikisha adhma yake ya kuifanya Ligi hiyo ya Vodacom kuwa ya kuvutiazaidi.Ligi hii tunataka kuifanya kuwa ni moja kati ya ligi zinazovutia na kuonesha ushindani barani Afrika, ingawaje ninajua kuwa kuna mengi ambayo yanatakiwa kuendelea kufanywa ili kuipa nguvu zaidi ligi hii”alisema Torrington.Alisema kuwa kwa kutambua hilo ndio maana Azam Media imehakikisha kuwa klabu zote zinapata fedha mapema ili kusaidia suala zima la maandalizi.
Azungumzia mikakati ya baadae
Akizungumzia mikakati ya baadae ya Azam Media alisema kuwa inatarajia kuanza kuonesha soka la mitaani (street soccer) mbalimbali moja kwa moja (live) itakayokuwa ikiendelea kwenye nchi za Kenya na Uganda. Alisema kuwa kwa sasa Azam Media imeanza kujikita katika nchi za Kenya, Uganda na Malawi ambapo itakuwa ikiuza ving’amuzi vyake katika nchi hizo.
Aliongeza kuwa pia katika kuhakikisha kuwa inatoa mwanya zaidi wa vipindi vizuri na vya kuvutia inaendelea na vipindi vya michezo vya Morning Trumpet, sport@8 pamoja na Kwetu House.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi, Mr SilasMwakibinga alisema kuwa kwa hatua hiyo ya Azam ya kuhakikisha upatikanaji wa fedha hizo kwa wakati ni nzuri na itasaidia kuzipatia timu muda mzuri wa kujiandaa.Alisema kuwa bodi yake inavutiwa sio tu na utangazaji wa vipindi unaofanywa na Azam bali pia hata nia yao ya kuendeleza soka la Tanzania.
Azam Media ilisaini mkataba wa miaka mitatu na wenye thamani ya TSHS 5,560,800,000 kuonesha mechi za live na za kurekodi mechi za Ligi Kuu na fedha hizo zinalipwa kwa awamu tatu
No comments
Post a Comment