HABARI ILIYOTIKISA JIJI,RAIS KIKWETE AVULIWA NGUO NA WANANCHI MCHANA KWEUPE.SOMA HAPA
| Wachokozi mada kwenye mdahalo huo,ambao umemalizika mda mchache uliopita,mwanzo ni Hawadhi Ally,wa pili ni Ayubu Liyoba,Onesmo Orenguluma,wa misho ni Profesa Mwisiga Baregu |
Na Karoli
Vinsent
WANANCHI
mbalimbali wamtaja Rais Jakaya kikwete kuwa ni kikwazo kikubwa cha upatikanaji
wa Katiba Mpya ,kutokana na kushindwa kusimammia misimamo yake mwanzo ambayo
ilikuwa inamalengo ya kupatikana katiba mpya ya Wananchi.
Hayo,yamegundulika mda huu kwenye Mdahalo
wakujadili Katiba mpya,uliondaliwa na Umoja wa Asasi za kirai
(AZAKI)uliofanyika jijini Dar es Salaam,mdahalo huo ambao uliwahusisha Wananchi
wa Kawaida pamoja na Wasomi Mbalimbali.
Katika
Mdahalo huo wananchi wameonekana Dhahiri kumshutumu Rais jakaya Kikwete
kwakushindwa kusimamia misimamo yake ya mwanzo ambayo ilikuwa inalengo la kupatikana Katiba mpya ya
Wananchi bila Upendeleo,ambapo sasa
ameonekana kubadilika na kuanza kushikilia Misimamo yake ya Chama cha Mapinduzi CCM, ambayo inakuwa kinyume na
sasa.
Kwa upande wake Msomi na mchambuzi wa
Masuala ya kisiasa Nchini kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Profesa
Mwisiga Baregu.alisema Rais kikwete amefanya usaliti mkubwa sana kwa wananchi
kwa kitendo chake kuanza kufuata maoni ya chama chake.
“Kiukweli mimi sikutegemea Rais kikwete
angefanya usaliti namna hii kwenye mchakato huu wakatiba, wakati mimi
sikutegemea .Kwanza wakati kila hatua tuliyokuwa tunaifanya kwenye mchakato huu
wakatiba tulikuwa tunamjulisha halafu na yeye alikuwa anaungana na sisi kwa
kazi tuliokuwa tuanafanya”
| WANANCHI WAKIWA MAKINI WAKISIKILIZA MDAHALO HUO |
“Lakini tunashangaa yeye amebadilika na
kuanza kufuata misimamo ya chama chake,na huku ndiko alipoanza kuharibu
mchakato mzima wa ujio wa Katiba mpya.Alisema Baregu.
Baregu,ambaye ni Kada kutoka Chama cha Demokrasia
na Maendeleo CHADEMA,alizidi kusema kitendo cha wajumbe wa Bunge Maalum la
Katiba kutoka Chama cha Mapinduzi CCM.
Kuendelea kujadili Rasimu ya Muundo wa Serikali mbili ni
kuvunja kanuni ya mabadiliko ya katiba kifungu cha 25,ambacho kinataka wajumbe
wa Bunge hilo kutojadili Rasimu ya Kwao.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la
katiba Nchini,Deus Kibamba,aliwataka wananchi kushirikiana na AZAKI ,kutetea
katiba yao na kutowaacha wanasiasa kuhodhi mchakato mzima wa Katiba.
Vilevile Mwanasheria na mwenyekiti wa
chama cha Wanasheria Zanzibar Hawadhi
Ally, ambapo yeye alikuwa miongoni mwa
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,alisema Rais Jakaya Kikwete ndio
mtu wa kulaumiwa kwa wananchi kwa kitendo chake cha kuanza kufuata matakwa ya
Chama chake ambao wamekuwa kinara wakubwa wakipinga maoni ya tume ya Jaji warioba.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi isiyokuwa ya
kiserikali,inasimamia Muenendo wa Shuguli za Bunge nchini,Marcus Albanile,aliwataka
wananchi kuacha upole wa kuigopo Serikali ya Rais Kikwete, ambayo imekuwa hikihalibu mchakato wa katiba
mpya na akawataka wananchi kuandamana na kulala barabarani na kudai katiba
mpya.
Ikumbukwe, Midahalo hii ya kuwapa wananchi
fursa ya kujadili katiba mpya imeandaliwa na Umoja Asasi zisizokuwa za Kiserikali AZAKI,ambao umoja huo
unawakilisha Asasi hizo zaidi ya mia tano.
No comments
Post a Comment