UCHAGUZI WA MALAWI AFRIKA KUSINI TUNA LA KUIFUNZA KAMA WATANZANIA: JUKWAA
Jukwaa la Katiba Tanzanaia (JUKATA) Limeamua kufunguka kuhusiana na chaguzi mbili za nchini Malawi na ile Ya nchini Afrika kusini na kusema kuwa katika Chaguzi hizo zote Chaguzi ambazo zinaonekana kuwa huru na haki ni ule wa AFRIKA KUSINI huku wakisema Chaguzi za nchini malawi iligubikwa na mizenge mbalimbali ikiwemo kiongozi mkuu wa nchi hiyo kuingilia mchakato baada ya kuona dalili za kushindwa,
Wakizungumza na Waandishi wa habari mapema hii leo jijini Daresaalam, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Ndg. Deusi Kibamba Amesema kuwa chaguzi za Malawi haikuwa huru hata kidogo kufuatia baadhi ya viongozi wa Nchi hiyo hususani, Rais Joyce Banda kuingilia mchakato wa uchaguzi na kuitaka Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kufuta matokeo ambayo yalianza kuhesabiwa ili uchaguzi urudiwe,
Amesema Jalibio la rais wa nchi hiyo kutumia madaraka yake kubadilisha mchakato huo ilionekana dhahiri pale alipoitaka tume ya nchi hiyo kufuta matokeo hayo ili mchakato urudiwe,
Kibamba amesema, Rias Banda alijaribu mara mbili kuhakikisha anabaki madarakani kwa kuiagiza tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kuhesabu upya tena kwa mkono kura zote ili aliyeshinda kiharali apatikane, hatua iliyotafsiriwa kuwa alikuwa anahitaji kujiongezea muda ili aendelee kuingoza nchi hiyo,
Hatua ya Jukwaa la katiba kutangaza kuwa chaguzi za Malawi ilikuwa na matatizo inakinzana na taarifa za waangalizi wa Ndani Toka AU na SADC ambao hivi punde walitoa taaarifa yao kuwa uchaguzi wa malawi ulikuwa shwari kwa mazingira ya nchi zetu za Afrika,
AU na SADC hawakusita kuonyesha furaha yao pale waliposema chaguzi zote za Afrika kusini na Malawi ulikuwa safi na hakuna matatizo ambayo wameyaona,
Akifafanua kwanini wao kama waangalizi wa nje walioenda katika nchi hzio kuangalia hali halisi ya uchaguzi, kupingana na matokeo ya wenzao wa AU na SADC, Kibamba amesema wao kama jopo lao linavyojulikana, huwa wanatumia kupima uhalisia wa mambo toka katika sehemu husika na si kwa viongozi wa nchi ama tume ya uchaguzi kwani kwa kufuata viongozi hao, utapata taarifa ambazo si sahihi kutokana na ukweli kuwa kila mtu huwa anavutia kwake,
Sisi tumeenda kule ndani kabisa katika vijiji vya Maria kuona hali halisi na hapo ndipo tumegundua kuwa uchaguzi hakuwa huru kwani baadhi ya kuratasi za kura zilikamatwa ziikiwa katika magari ya magereza na haikujulikana ni wapi karatasi hizo za kura zilikuwa zikipelekwa,
- MaZINGIRA YA KUFANYA KAZI KWA TUME YA UCHAGUZI HUKO BONDENI YALIKUWA RAFIKI KWA WAFANYAKAZI WAO , HIVYO MORALI YA KUSIMAMIA KURA ILIKUWA JUU UKILINGANISHA NA MALAWI AMBAKO WATUMISHI KATIKA ZOEZI ZIMA LA KUPIGA KURA WALIKUWA WANALIA NJAAA
- UHURU WA KUKUBALIKA KWA TUME YA UCHAGUZI, aFRIKA KUSINI INA TUME HURU KISAWASAWA, LAKINI HUKO MALAWI NI TATIZO,
- LUGHA ZA KASHIFA ZILIKUWEPO .
No comments
Post a Comment