KAULI,YA LOWASSA SASA YAITESA CCM,SOMA HAPA UONE JINSI TANZANIA INAVYOFUATA NYAYO ZA NCHI YA NIGERIA
Hao ni
miongozi mwa maelfu ya vijana waliojitokeza jana katika usahili wa Jeshi
uhamiaji,uliofanyika uwanja wa Taifa jijin Dar es Salaam,huku jehi hilo
likiitaji watu 70 tu,
|
Na Karoli Vinsent
KAULI aliyoisema Waziri Mkuu
aliyejiuzuru Edward Lowassa kwamba vijana wasiokuwa na Ajira ni Bomu
linalosubili kulipuka mda wowote,linazidi kujidhihilisha, Baada ya leo Maofisa
wa Uhamiaji kuonja kali ya mwaka, ambayo hawataisahau maishani mwao.
Hayo yalibuka Jana Kwenye Usahili wa
Vijana ambao waliomba nafasi ya kujiunga Jeshi la uhamihaji nchini kwa
mwaka huu,ambazo zilifanyika kwenye uwanja mpira wa Taifa Jijini Dar es
Salaam,ambapo vijana hawo walikuwa wengi na kujaza uwanja huo kama kuna
mechi ya mpira ya Watani wa jadi Simba na Yanga,ambayo imekuwa ikijaza watu
kiasi hicho.
Mwandishi wa Mtandao huu, alifika
eneo hilo ndipo alishudia kundi la watu likiwa likisubili kufanyiwa
usahili,huku vijana hao wakiwa wamechoka kwa kuwangojea maofisa hao ili waje
kuwapa mitahani ambayo wanaitumia kwenye usahili.
Ambapo vijana hao wakitoa malalamiko
kwa maofisa hao wa uhamiaji kwa kuwa weka kwa mda mlefu.
“Kama wanachakachua hayo majina
waseme tu,maana tumekaa mda mrefu sana hapa, akuna chochote
kinachofanyika”alisema kijana mmoja ambaye aligoma kutaja jina lake mtandaoni
Kwa upande wake kijana mwengine
aliyetambulika kwa Jina Moja la Juma naye alionekana kupata wasiwasi kuhusu
upatikanaji wa ajira hiyo kwenye jeshi hilo ambalo ni la muhimu katika Taifa
letu.
“Jamani hivi mimi sina bahati na
soko hili la Ajira la Tanzania nimezunguka na vyeti vyangu zaidi ya miaka
miwili nakosa kazi hivi haka “kadegree” yaani Shahada yangu ina nini
jamani mbona nateseka hivi”alisema Juma
Mwandishi wa Mtandao huu alipotaka
kupata ukweli kutoka kwa maofisa hao wa Jeshi la Uhamiaji kuhusu shutuma
hizo,ambapo alijitokeza Ofisa mmoja ambaye akutaka kutaja jina lake kwa kusema
yeye sio Msemaji wa Jeshi la Uhamiaji.
“Hatuna Jinsi sisi ndugu
mwandishi,kumbukeni pia na sisi binadamu hebu wewe ungekuwa kuwa sisi
ungefanyaje,maana watu ni wengi sana nchi hii hawana Ajira,na tumefanya kazi
kubwa sana kuwapunguza”
“Kwani watu waliomba zaidi ya Laki
mbili,tena tumewapunguza mpaka wakamebaki kiasi ambacho tunaweza kukimudu,na
hawa wenyewe unaowaona tumewagawa kimakundi wengine wamekuja leo “Ijumaa”na
wengine tumewapangia tarehe 16 mwezi huu,hali ni mbaya sasa kaka Ajira hakuna
watu wanachanganyikiwa tu hao”alisema ofisa huyo
Mwandishi alipotaka kujua nafasi
hizo ambazo idara hiyo ni watu wangapi,ofisa huyo alisema waitaji
watu 70.
Uchunguzi wa Mwandishi wa Mtandao
huu,umebaini idadi ya watu waliofika tu kwenye usahili wa kwanza ni zaidi ya
elfu ishirini huku kukiwa na hatua nyingine ya usahili itakayofanyika jumatatu
ijayo,ambayo nayo itakuwa na watu wengi zaidi ya hiyo.
Vijana hao waliojitokeza kwenye
usahili huo, ni miongoni mwa waliomaliza kutoka vyuo vikuu
mbalimbali nchini,ambao wanye ngazi ya elimu kwaanzia Diploma hadi shaada ya
pili .
Naye msomi na mchambuzi wa Masuala
ya Kisaisa kutoka chuo Kikuu cha Dodoma,Seiph Yahaya alisema kwa sasa Serikali
inahaja ya kutafakali kauli ya aliyoisema Edward Lowassa,kuhusu kauli yake ya
ukosefu wa Ajira kwa vijana.
“Kikuweli mimi nakwambia hili ni Bomu
tu linalosubili kupasuka mda wowote tu,sahivi hali ni mbaya sana hususani
linapofikia suala la Ajira inakuwa balaa na yote haya ndugu yangu ni Makosa
yalifanywa na Serikali hii,haiwezekani wamalize Viwanda vyote kwa kuviua”
“utategemea nini sasa,kama serikali
ingewekeza kwenye viwanda vyandani sidhani tatizo lingekuwa kubwa kama sasa
kama hivi ilivyokuwa kubwa,na lazima hili litakuwa Bomu tu”alisema Seiph Yahaya
Hakuna maoni
Chapisha Maoni