Jumuiya ya wanafunzi wa kiislam NIT wawapigia magoti wadhamini, ni kuhusu ujenzi wa msikiti mpya chuoni hapo
Mmoja wa viongozi shupavu katika chuo hicho akipokea cheti chake toka jumuiya ya Kiislam Msanit wakati wa mahafari hayo |
Jumuiya ya kiislam, katika chuo cha taifa cha usafirishaji NIT (MSANIT) wametoa wito kwa muislam yeyote na hata yule ambae hajabahatika kuwa muislam kujitolea kwa moyo wa dhati ili ujenzi wa mskiti katika chuo hicho uchukue hatua zake,
Wakizungumza na mtandao huu hivi karibuni katika mafahari ya jumuiya hiyo, mmoja wa maamiri mkubwa kabisa wa ngazi ya juu ambaye amesita kutoa jina lake hadharani, amesema kwa sasa jumuiya yake inatatizo kubwa la kifedha ili kujenga msikiti ambao kwa muda mrefu ramani yake tayari imeshakamilika
Amiri amesema, hatua zote za awali tayari zimeshakamilika na kwamba kitu kikubwa ambacho kwa sasa kinasumbua ni upatikanaji wa fedha za kuanza ujenzi mara moja,
Sisi tunaomba watusaidie katika kujenga huu msikiti kwani waislam ndo kwanza tunaongezeka hapa chuoni huku msikiti uliobo bado ukiwa hauna uwezo wa kubeba waumini wote, tunaona kama udhamini wa ujenzi wa msikiti utakamilika mapema basi kuna dalili nzuri ya waislam kupata sehem ya kuabunia bila matatizo yoyote.
Akijibu maombi yao, mgeni mualikwa aliwaahidi matofari ya ujenzi wa msikiti huo, huku akiwataka wafanye tathimini mapema ili kujua gharama halisi za matofari katika ujenzi huo.
Mimi kwanza kabisa niseme nitachangia matofali, lakini msibweteke katika hilo kwani waislam tuko wengi na kama mtalisema hilo hadharani basi mtasaidiwa, aliongeza huyo mgeni mwalikwa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni