YONNA AIBOMOA CHADEMA, AHOJI UHALALI WA MUUNGANO WA UKAWA, ASEMA HABIBU ZA REJEA ZIKO WAPI?????
Yonna amesema hatua ya kutoridhishwa kwa baadhi ya wanachama wa Chadema inakuja kufuatia ukweli kuwa, viongozi wa ngazi ya juu walijaribu kuwaaminisha wanachama wa Chadema kuwa Vyma vya CUF na vingine hapa nchini ni baadhi ya mapandikizi ya Ccm hivyo kuungana nao ni sawa na kuua kasi ya mapinduzi katika nchi hii,
Amesema kama viongozi hao waliwatukana wenzao wa Cuf na vyama vingine leo hii iweje vyama hivyo vionekane vinafaa katika siku hizi za karibuni, Alihoji Bw. Yonna,Je ndoa Ya ccm N a Cuf imevunjiaka? na ni lini ndoa hiyo imevunjika?,
amesma Chadema wamekuwa wakiwaamisha wanachama waake kuwa Mwenyekiti wa Nccr mageuzi ni pandikizi la Ccm, na ndio maana amechaguliwa na Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuingia bungeni, Je Hivi hiyo ndoa ya CCM na Nccr mageuzi imevunjwa lini na wapi??? alihoji Bw. Yona,
| Hapa Yonna akisoma Tamko la kupinga uhuni wa kisiasa unaitwa ukawa mapema hii leo, Yonna anadai kundi la ukawa ni sawa na kikundi cha sudani kusini chenye nia ya nchi kutotawalika, |
Akizungumzia hatua za ukawa kususia bunge, Mwenyekiti huyo amedai kuwa hatua hiyo wanaikemea vikali kwani uwanja wa kujenga hoja ni bungeni na hatua ya kutoka ni sawa na kuogopa mambano,
Ameshauli viongozi hao kulea bungeni ili katiba mpya iandikwe na kama hawatalejea basi wao watakuwa na lakujibu kwani fursa ya kuandika katiba mpya tumeidai kwa muda mrefu lakini tulikuwa hatuipati lakini sasa tumeipata ni vyema tukaitumia ipasavyo.
Amesema wakiona hawawezi kabisa basi watangaze nafasi zao ili tufanye uchaguzi wa kuwapeleka watu watakaotetea taifa hili, kwa nguvu zao zote na sio watakaoendeshwa na misingi ya kimaslahi yao binafsi.
No comments
Post a Comment