Zinazobamba

VIDUKU, VIGODORO SASA ZAPIGWA MARUFUKU, "KISA NI PANYA ROAD WANAOSUMBUA JIJI"

Kamishina Suleiman kova akionyesha picha ya viongozi wa Panyaroad waliokamatwa hivi punde, kamanda kova Ametangaza kukamatwa kwa panyaroad wapatao 149 kupia msaada wa wananchi na viongozi wao ambao walibanwa kisawasawa ili kutoa taarifa za kundi hilo (picha@24)

Ili kukabiliana vizuri na kundi la uporaji linalojiita Panyaroad, jeshi la polisi kanda maalum ya Daresalaam limetangaza kupiga marufuku ngoma za usiku zinazotambulika kwa majina ya Kangamoja, Baikoko na ngoma maarufu ya Kigodoro, ambayo amesema kwa kiasi kikubwa ngoma hizo zinachanga kuzalisha makundi ya panyaroad.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo,Kamishna wa polisi Kanda maalum Ya Daresaalam, amesema kwa operation iliyofanyika katika maa 48 yaliyopita imebaini wazi kuwa chacho za makundi haya ya uporaji yanatokana na miziki ya usiku.
Kova amesma, Watu wanaojishughulisha na miziki hiyo maranyingi wamekuwa ni watmiaji wa madawa ya kulevya kama, Bang, Unga N kujidunga sindano, ambapo wakishamaliza kutumia madawa hayo, ndio wanajiunga makundi na kupita katika makazi ya watu na kuwaanza kupora mali za watu wasio na hatia,
Hawa ndio wazee wa panya road wanaofanya wakazi wa maeneo ya tabata, mabibo, Luhanga, Mmburahati na eneo lote linalozunguka bonde la mto msimbazi wasilalae


Kova amesma tayari tunafanya mkakati wa kuwasiliana na wenzeu wa utamaduni ili waacha kabis akutoa vibari vya shughuli za usikuu kwani mara nyingi shughuli hizo zinazalisha waporaji ambao wanatia hasara za mali kwa watu wasiohusika na shughuli husika

Hizi ngoma za michiriku, minanda, Viduku, Kangamoja, Baikoko zinachangia sana uwepo wa panyaroad. sasa hatutaruhusu. Alisema

Katika hatua nyingine, kamanda kova ametoa wito kwa wazai kuacha kuwakimbiza watoto wao nje ya Daresaalam kwa kuhofia kukwamatwa na badala yake watumie muda huo kuwapa elimu watoto wao waachane na makundi yasiyo na maana na wawape somo la kuanzisha biashara ili wafanye kazi na kujipatia kipato,

Kova amesema, tunataarifa kuwa wazazi wa watoto hawa panyaroad, wanafanyamipango ya kuwakimbiza watoto wao nje ya Daresalaam ili wasikamatwe na mkono wa sheria, tunasema hao watoto hata waende nje ya Tanzania jeshi la polisi linauwezo wa kuwakamata popote pale walipo, tunachowashauri ni bora wakatumia fedha hizo kuwapa mitaji na wakajishughulisha na kazi zingine
"Jeshi ni moja hilihili hata uende wapi tunaweza kukukamata, Tunaweza kukama gari hata iwe Mwanza kuliko wewe ambae unajulikana chanzo chako" ALIONGEZA KOVA

No comments