operation tokomeza :panyaroad" yakamata kundi la watu 155 mpaka sasa, wapo viongozi wao wakuu sita na wafuasi wao 149, kova asema kazi bado inaendelea, Apiga stop Vigodoro na Ngoma za Usiku
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
26/05/2014
POLISI KANDA MAALUM LIMEFANIKIWA KUWAKAMANDA
VIBAKA MAARUFU KWA JINA MBWA MWITU AU PANYA ROAD WAPATAO 149 KWA MUDA WA MASAA
24 YALIYOPITA.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanya
msako wa nyumba kwa nyumba, mtaa na maeneo yaliyoathirika kwa hofu ya vijana
ambao ni vibaka maarufu kama Mbwa mwitu
au Panya Road. Msako huu uliofanyika
ndani ya masaa 24 hadi alfajiri ya tarehe 26/5/2014 kwa lengo la kuwaondolea
hofu na uhalifu dhidi ya makundi ya vijana wadogo wasio na ajira ambao uliibuka
hivi karibuni.
Maeneo yaliyoathirika ni Kigogo, Magomeni, Tabata,
maeneo yote yanayozunguka mto Msimbazi, maeneo ya Mbagala nk. Msako huu unaendelea kufanywa na askari wa
vikosi maalum ambao wamepewa kazi ya kuhakikisha kuwa vikundi hivyo haviibuki
tena na vinatokomezwaa kabisa kwa kuwakamata
wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kuvamia kwa mkundi wananchi ambao
hawana hatia
Kati ya watuhumiwa 149 waliokamatwa mmoja
amegundulika kuwa ni kiongozi aitwaye ATHUMANI SAIDI miaka 20, Mkazi wa Kigogo
na amekiri anaongoza kundi la watu zaidi ya 15 ambao baadhi yao ni kati ya
waliokamatwa. Imegundulika pia kwamba
vijana hawa wanatumia dawa za kulevya aina ya bangi na wengine hujichoma
sindano na kuwafanya iwe rahisi kujihusisha na matukio ya uhalifu. Vijana hao hupenda kushiriki katika ngoma
kama Mnanda, Mchiriku, Kigodoro, Kanga moja nk. ambazo kwa kawaida huchezwa
hadi usiku wa manane. Wakitoka katika
ngoma hizo hujikusanya pamoja na kufanya matukio ya uporaji kwa mtu
wanayekutana naye, kufanya uvunjaji katika majumba na wakati mwingine wana
mtindo wa kugema mafuta ya diesel au petrol katika matanki ya malori
yanayosafirisha mafuta. Operesheni kali
inafanyika katika maficho ya wahalifu hao ikiwa ni pamoja na daraja la River
side, Kigogo darajani, Manzese, maeneo ya Tandale pamoja na maeneo mengine ya
maficho mkoa wa Kipolisi Temeke.
Zipo taarifa kwamba baadhi ya wazazi wasio
waaminifu wamewasafirisha watoto wao wahalifu katika makundi haya kwenda
mikoani ili kukwepa wasinaswe na msako huu mkali. Hata hivyo Jeshi la Polisi lina mtandao wa
kutosha kati yake na mikoa mingine na nchi jirani hivyo litawatafuta popote
walipo na kuwakamata.
Oparesheni hii ni endelevu na ya kudumu hadi kero
hii ya vibaka itakavyokwisha kabisa. Baadhi ya majina waliokamatwa ni kama
ifuatavyo:-
1.
DANIEL PETER @
MALUNDE, miaka 25, mkazi wa Yombo Kigunga
2.
MWISHEHE ADAM,
miaka 35, mkazi wa Mtoni mashine ya maji
3.
MOHAMED SAID,
miaka 32, mkazi wa Mtoni
4.
JAKAMA
ALPHONCE, miaka 23, mkazi wa Mtoni Kilakala
5.
HAMADI MDUDU,
miaka 25, mkazi wa Mbagala
6.
SALUM MUSA,
miaka 25, mkazi wa Kiwalani
7.
ANTHONY DANIEL,
miaka 20, mkazi wa Mashine ya maji
8.
FIDELIN
ANTHONY, miaka 18, mkazi wa Kigogo
9.
HAMZA MAZUMA,
miaka 19, mkazi wa Kigogo
10. MGANGA ABEID, miaka 20, mkazi wa Kigogo
11. SAID ABEID, miaka 19, mkazi wa Kigogo
12. SALUM NYENJE, miaka 36, mkazi wa Chamazi
13. DOMINICK PETER miaka 22, Mkazi wa Kigogo
14. KULWA ABEID, miaka 20, mkazi wa Mabibo
15. MUSA IBTRAHIM, Miaka 20, mkazi wa Magomeni
16. HUSSEIN SHABAN, miaka 22, Mkazi wa Magomeni
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR
ES SALAAM
No comments
Post a Comment