Zinazobamba

KAMANDA KOVA AUNGANA NA JK KUTOA RAMBIRAMBI MSIBA WA MWANDISHI, CHADEMA NAO WASIKITISHWA


 
 Kamishina wa polisi kanda maalum ya Daresaalam ameungana na mienendo ya rais wa nchi. Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuunga mkono na kutoa rambirambi yake kama kamanda jumla ya Tsh: 100,000 ikiwa kama sehemu ya rambirambi yake ya kujali mchango aliokuwa akiufanya mwandishi nguli wa TV Mlimani

Akikabidhi rambirambi hiyo kwa mmoja wa waandishi wa habari,. Kamanda Kova amemuelezea mwandishi huyo kama mwandishi shupavu, alimjeshi ambae alikuwa akijulikna na kila mtu ambae anafanya nae kazi
Hakika tumesikitisha sana sisi kama jeshi la polisi kwa kifo cha Mwandishi huyu, tumepoteza mtu muhimusana ambaye katika tasnia ya habari halikuja kuzibika aliongeza Kamishina kova,

Nao, Chama Cha Chadema kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano na Uhusiano ya Chama cha Demokrasia naMaendeleo (CHADEMA), imepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa zakifo cha mmoja wa waandishi wa habari za picha (mpiga picha) mwandamizinchini, Maximillian John Ngube aliyefariki siku ya Ijumaa baada yakuugua muda mfupi.
 
Kwa masikitiko makubwa kurugenzi, kwa niaba ya chama, inatuma salaam zapole kwa familia ya marehemu Maximilian kwa kuondokewa na baba nampendwa wao, katika wakati ambao tunaamini walikuwa badowakimhitajisana kama moja ya nguzo za familia.Kurugenzi pia inatoa salaamu za pole kwa wafanyakazi wa Mlimani MediaHouse, (inayomiliki Mlimani Tv, Radio Mlimani na Gazeti la The HillObserver), ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shule Kuu ya Uandishi waHabari na Mawasiliano kwa Umma, ambako Maximilian alifanya kazi nakutimiza wajibu wake kwa jamii kama mwandishi wa habari, hadi mauti
yalipomkuta.
 
Salaam hizi za rambirambi pia zinatolewa kwa waandishi wa habarinchini, kwa kumpoteza mwandishi mwenzao, mmoja wa wapiga picha wakongwe,katika wakati ambao uhodari wake na utayari wa kujituma kwa ajili yaubora wa kazi yake na chombo chake, hatimaye tasnia nzima ya upashanaji
habari, ulikuwa bado ukihitajika kweli kweli.


Tunajumuika pamoja na familia, waandishi wa habari nchini na wengine wote waliowahi kufanya kazi naye, bila kusahau Watanzania wotewalioguswa na kifo cha Maxi (kama alivyojulikana kwa watu wengi), ambaotunajua hata kama hawakuwa wakimjua Maxi kwa sura, lakini wamenufaika namatunda ya kazi zake nzuri katika vyombo vya habari mbalimbali nchini alivyowahi kuvifanyia kazi.Kifo cha Maxi, si kwamba kimeacha pengo kubwa kwa familia yake na kazini kwake pekee, bali kwa tasnia nzima ya uandishi wa habari nchini. 

Maxi alijulikana sana miongoni mwa waandishi na ‘sources’ wake nahatimaye jamii nzima, atakumbukwa zaidi kwa mambo matatu, uhodari(ubora) wa kazi zake, ucheshi na alivyokuwa mwalimu wa vijana wengi
ambao kwa kupitia mikononi mwake, wamekuwa watangazaji wa habari auwapiga picha wazuri na hodari kama alivyokuwa Maxi, ambao wamesambaa kwenye vyombo mbalimbali nchini.

Hakuna mtu aliyemjua Maxi asiujue ucheshi wake! Hakuna mtu aliyewahikumshuhudia Maxi akiwa kazini, ambaye asingejua ndani ya muda mfupi kuwayule aliyekuwa mbele yake, akihangaika huku na kule, hapa na pale,kutafuta ‘angle’ au ‘shot’ nzuri, alikuwa ni mwandishi anayeipendataaluma na kuithamini kazi yake.
 
Kwa watu waliofanya kazi na Maxi katika majukumu yake, kama waandishiau vyanzo vya habari au waliomfahamu kupitia maisha yake ya kawaida,hakuna maneno yatatosha kumalinza simanzi ya ghafla waliyoipata kwakuondokewa na ‘mpiganaji’ huyu, ambaye pamoja na kufa kimwili, sifa namatendo yake katika tasnia ya habari yataendelea kudumu.

Tunawaombea wote walioguswa na msiba huu, Mwenyezi Mungu awatie nguvuna kuwapatia moyo wa subira wakati huu wa majonzi mazito ya kuondokewa na mpendwa, Maxi.

Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi Maxi.
Imetolewa leo Jumamosi, Mei 24, 2014 na
Tumaini Makene-Ofisa Habari Mwandamizi*Kny; Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano- CHADEMA

No comments