SASA BENKI YA DAMU YAISHIWA , MAHITAJI HALISI NI LITA 400,000 ZILIZOPO NI LITA 160,000 VIONGOZI WA DINI WAPIGIWA "MAGOTI" KUNUSURU TATIZO

Hatimaye wasimamizi wa benki ya damu hapa nchini wameamua kufunguka na kueleza ukubwa wa tatizo la Damu hapa nchini na kusema kwa sasa taifa liko katika wakati mgumu kutokana na benki ya taifa kuishiwa na Damu na hivyo kuhatarisha maisha ya Watoto na wamama wajawazito ambao ndio watumiaji wakuu wa damu hiyo
Akizungumza na waandishi wa habari afisa mkuu toka NBTS Bw. Paul Mhame amesema kuwa tatizo la damu sasa limekuwa ni tishio kubwa na hivyo kutia hofu kwa wamama wajawazito ambao hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua kupoteza maisha yao,

Amesema mahitaji ya nchi kwa sasa ni jumla ya lita laki nne, wakati benki ya damu yenyewe ina jumla ya lita laki moja na sitini hali ambayo inaonyesha taa nyekundu kwa wagonjwa wanaohitaji damu pindi wanapokuwa wagonjwa,
Kufuatia tatizo hilo, tayari wameanza kuchukua hatua mbadala kwa kuwaita viongozi wote wa dini hapa nchini na kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kuchangia damu salama kwa hiyari ili nao wawe mabalozi wetu wa kuwahubiria wafuasi wao juu ya kuchangia damu katika benki ya taifa ili kutatua tatizo lilolopo,
Ukiangalia tatizo jinsi lilivyo, utaona ni jinsi gani kunahitajika hatua za haraka kuchukuliwa, wamama wajawazito wamekuwa wakipoteza maisha yao kutokana na ukosefu wa damu katika mabenki zetu hivyo kama watanzania watakuwa tayari kuchangia damu kwa hiyari basi kuna uwezekano wa kuondoa tatizo hili kwa asiliia kubwa,

Umoja wetu ni nguzo muhimu sana katika kuondoa Changamoto zinazokabili taifa hili, Lita laki nne si kitu kwa watanzia milion 45.5 tunapaswa tuoneane huruma tujitowe ili kunusuru maisha ya wenzetu alisema shehe mkuu wa mkoa Alhadi Mussa ambaye ni mmoja wa viongozi waliohudhulia Tatizo hilo,

Miongoni mwa Changamoto ambazo zimetajwa kwa watanzania kuogopa kutoa damu yao ni kutokana na kuogopa kujua kama wameathirika na virusi vya ukimwi na wale wengine wamekuwa hawana uelewa mkubwa juu ya faida za kuchangia damu kwa hiari,
Ametoa wito kwa watanzania kuanza kujenga tabia ya kujitolea damu ili kunusuru maisha ya watu.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Kutoa Damu ni Salama na Hakuna Maumivu
Kwa wakazi wa Dar mnakaribishwa katika kituo cha kanda ya mashariki Ilala mchikichini mtaa wa max mbwana, pia unaweza kwenda kituo kidogo cha mnazi mmoja karibu na kituo cha afya mnazi mmoja kwa maelezo zaidi piga 0712612000 au au tembelea ukurasa wetu wa twitter
https://www.twitter.com/ ChangiaDamuTz Tovuti yetu http://www.nbts.go.tz/ na http:// changiadamutz.blogspot.com/
Kwa wakazi wa Dar mnakaribishwa katika kituo cha kanda ya mashariki Ilala mchikichini mtaa wa max mbwana, pia unaweza kwenda kituo kidogo cha mnazi mmoja karibu na kituo cha afya mnazi mmoja kwa maelezo zaidi piga 0712612000 au au tembelea ukurasa wetu wa twitter
https://www.twitter.com/
No comments
Post a Comment