Zinazobamba

BOKO HARAM MPYA YATIA TIMU BONGO, NI HAWA WA KUITWA SURA MBAYA, PANYAROAD NA MBWA MWITU, WAFUNGA SHUGHULIZA UZALISHAJI KINONDONI KWA MUDA, IFUATE HAPA KWA HABARI ZAIDI

NAFAFANUA, Kamishina wa polisi kanda maalum ya Daresalaam akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Picha na maktaba.
 Unaweza kusema ni Boko haram mpya ndani ya Bongo imeingia,  HAWA WA KUITWA BADFACE NA PANYAROAD WASIKIENI TU HIVYO2, Nilikuwa Maeneo hivi Pande Za Luhanga,ghafla Tukaanza Kusikia Mayowe , Raia Wakaanza Kukimbia Hovyo,maduka Yakaanza Kufungwa,sekunde Chache Kupita Mara Nikaona Kundi Kubwa La Watu Sio Chini Ya 200 Wakiwa Na Mapanga, Virungu Wengine Wakiwa Na Masime, Dah, Yaani Nilishangaa Kuona Vtendo Wanavyofanya,ni Zaidi Ya Boko Haram,hakupona Mtu Wala Maduka,raia Wamebaki Kuchungulia Madirishani, Hakika Amani Imetoweka Luanga,na Mburahati, Hayo si maneno yangu ni maneno ya mkazi mmoja wa Kata ya Luhanga wakati akitoa ushuda wake kwa mwandishi wa habari hizi huko nyumbani kwake maeneo ya Luhanga karibu na Festini,

Akizungumza nami hiyo jana , Bw. Jumanne hasani amesema kundi kubwa la vijana ambao umri wao unakadiriwa kuwa kati ya miaka 9 had 19 wamekuwa ni gumzo kubwa kwa tabia yao ya kujichukulia maamuzi ya kupora maduka, kupiga watu hovyo, tena kwa kutumia dhana kali za mapanga,


Fullhabari ilifika eneo la tukio na kujionea jinsi watotohao wa Mbwa wanavyotekeleza kazi yao kiustadi huku wakitumia mapanga na masime,hali iliyowarahishia wao kuchukua mali za raia kwa kadri ya wanavyotaka,

Watoto hao ambao ni takribani mwezi sasa wamekuwa ni tishio kwa shughuli za uzalishaji kwa maeneo ya mburahati na Luhanga, kutokana na Amani katika maeneo hayo kutoweka kabisa, inasadikika watu hususani wauza maduka wamekuwa wakifunga madka na kufungua maduka hayo kwa tahadhari ya hali ya juu wakiogopa kufilisiwa mali zao.
Wadadisi wa mambo wanasema kama hatua za makusudi hazitachukuliwa dhidi ya watoto hawa wanaonekana kuwa tishio la amani katika maeneo hayo, hakuna shaka kuwa Tanzania tunazalisha boko haram wapya ndani ya kipindi kifupi kijacho,
Wanasema, itafika wakati watu watachoka na vitendo vinavyofanywa na watoto hao na ndipo wananchi watachukua sheria mikononi kwa kuwaadhibu wenyewe hatua inayodaiwa kuwa ni mbaya kwa mustakabali wa taifa,
Wanasema, ikifika hatua ya wananchi kuuana wenyewe kwa wenyewe hapo ndipo vita ya wenyewe kwa wenyewe itakapotokea na hivyo nchi kuingia katika machafuko

No comments