WAZIRI AIPONGEZA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA,

Alisema lengo la kuongeza idadi ya safari hizo ni kutokana na uwapo wa vivutio bora vya utalii kwenye maeneo hayo .
Nyalandu alisema kurejea kwa ndege ya shirika hilo katika njia hizo kutakuza sekta ya utalii na kurahisisha uunganishwaji wa maeneo hayo muhimu yenye vivutio vikubwa nchini.
"Nimekuwa miongoni mwa abiria wa kwanza kusafiri kwa ndege hii kuja Arusha. Kwa hiyo nataka kuwahakikishia wote kuwa usafiri wa Air Tanzania ni tulivu, huduma nzuri ni salama,'' alisema Nyalandu
Katika uzinduzi huo, Nyalandu alilitaka shirika hilo la ndege kuhakikisha linatimiza dhamira yake ya kweli na kuongeza ushindani kati
ka sekta ya usafiri wa anga nchini ili waweze kurejesha imani waliyonayo abiria wake wengi.
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa ATCL, Juma Boma alisema safari ya Dar es Salaam – Arusha – Zanzibar ni sehemu ya mkakati wa shirika wa kutanua huduma katika maeneo mengi iwezekanavyo.
Alisema lengo la shirika hilo ni kuendelea kutoa huduma zenye gharama nafuu, vilevile kuongeza uwezo wa abiria kusafiri kwa wakati wao.
Waziri wa Zanzibar, Mwinyihaji Haji Makame, alisema inatia moyo kuona ATCL ikirejesha safari zake Zanzibar baada ya kusitisha huduma miaka minne.
na kuwataka kufuata muda na kuhakikisha wanapunguza adha ya usitishaji wa safari endapo wanataka kurejesha imani miongoni mwa abiria walio wengi.
Akizungumza baada ya kupokea safari hiyo ya uzinduzi katika Uwanja wa Ndege Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, John Mongela alisema, uanzaji wa safari hizo za ATCL katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Geneva ya Afrika umerejesha sifa iliyokuwa nayo ndege hiyo ya taifa kipindi cha nyuma wakati wa mikutano ya kimataifa jijini hapa.
"Hii ni hatua ya busara kwa ATCL. Jiji la Arusha halitoi tu fursa ya ndege hii kusafirisha watalii moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kuja Arusha na kuwaunganisha kwenda Zanzibar bali pia inawapa fursa ya kusafirisha viongozi wa kimataifa wanaosafiri mara kwa mara kuja Arusha kwa ajili ya mikutano," alisema.
No comments
Post a Comment