MKURUGENZI AWAPIGIA MAGOTI "WANANCHI" HUKO SONGEA
Wanachi wa mkoa wa Ruvuma Mjini Songea wamehakikishiwa kupata umeme wa uhakika ifikapo wiki ijayo na kwamba yote ambayo yametokea na usumbufu ambao wameupata shirika linaomba radhi na kuhaidi kuwa sasa watapata umeme wa uhakika,
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo,Naibu Mkurugenzi wa Uzalishaji wa umeme, Eng. Boniface S.Njombe, kuanzia wiki ijayo sasa umeme katika mji wa Songea utapatikana kwa uhakika, kwani kifaa ambacho kilichokuwa kimeharibika kitakuwa kimeshakamilika kutengenezwa,
Amesema tatizo kubwa la mgawo wa umeme katika mji wa Songea ni kuharibika kwa kifaa cha Table Chager ambacho kinauwezo wa kukandamiza hewa ili kutengeneza umeme unaotumiwa na wakazi wa mji wa Songea,
Amesema, kuharibika kwa kifaa hicho kumesababisha uwezo wa kusambaza umeme katika mji huo kushuka kutoka katika mahitaji halisi ya 4.1Megawati hadi kufikia 3.1Megawati ikiwa ni pungufu la 1.1m hali iliyosababisha kwa mgawo wa umeme katika jiji hilo tokea april 06 mwaka huu
Eng. Njombe amesema tayari jitihada za matengenezo ya kifaa hicho kilichoharibika yameshachukuliwa na kwamba hivi tunavyozungumza kifaa hiko tayari kimeshafanyiwa matengenezo hapa jijini Daresaalam katika Kituo Cha Mantrac ambao kwa ukanda huu wa Afrika mashariki ni wao pekee wenye mamlaka ya kutengeneza kifaa hicho,
"Tayari kifaa kimeshaenda mjini songea na mafundi wetu wapo huko, walikifunga kifaa hicho lakini kulitokea matatizo ya kiufundi na hapo ndipo kifaa hicho kilishindwa kuzalisha umeme wake wa kawaida hatua iliyolazimisha kukifungua tena na kuwaita wenzetu wa mantrac ili waweze kwenda kukifunga na kianze kufanya kazi, na hivi tunavyozungumza tayari mafundi hao wa mantrac wako huko ili kukamilisha majukum yao na tunauhakika zoezi litakamilika wiki ijayo" Alisema Eng. Njombe.
Aidha katika hatua Nyingine, Njombe amekanusha habari iliyotolewa na gazeti moja la kila leo kuwa Tatizo la mgao wa umeme Mjini Mjini Songea linazaidi ya miezi minne sasa, na kusema taarifa hizo si sahihi kwani tokea kutokea tatizo hilo mpaka sasa ni takribani wiki tatu.
Amesema wakati mwingine ni vizuri kupata taarifa kutoka katika Chanzo kinachoaminika kuliko kuandika habari ambayo uhakika wake ni mdogo
No comments
Post a Comment